Mbunge
wa Monduli na Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa akiwasalimia mamia ya
wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu mkoa wa Dodoma, waendesha boda boda
na wamachinga wa mkoa huo walioandamana hii leo hadi nyumbani kwake Area
D mjini Dodoma kumuomba pindi wakati ukifika kwa mujibu wa taratibu za
chama cha Mapinduzi (CCM) asisite kuchukua fomu ya kugombea nafasi ya
Urais.
Lowassa amesema anazidi kuhamasika kufuatia maombi ya watu wa makundi mbalimbali ya jamii wanao muomba kugombea urais mwaka huu.
Aidha na yeye amewaomba vijana hao na makundi mengine kuwahimiza wenzao vyuoni na hata mitaani kujitokeza kwa wingi kujiandikisha katika daftari la wapiga kura ili siku ya uchaguzi wawe na sifa za kuweza kushiriki katika uchaguzi kwa kupiga kura.
Aidha na yeye amewaomba vijana hao na makundi mengine kuwahimiza wenzao vyuoni na hata mitaani kujitokeza kwa wingi kujiandikisha katika daftari la wapiga kura ili siku ya uchaguzi wawe na sifa za kuweza kushiriki katika uchaguzi kwa kupiga kura.
Rais wa serikali ya wanafunzi akizungumza
Mheshimiwa Lowassa akizungumza na wanachuo hao
Wanafunzi
hao zaidi ya 300 walifika nyumbani kwake hapo majira ya saa sita mchana
na kuzungumza nae na kufikisha salamu zao ikiwa ni pamoja na kumchangia
fedha za kuchukulia fomu.
Aidha
Lowassa kwa Upande wake amewashukuru vijana hao na kusema kuwa ujio wao
na ule wa masheikhe wa Bagamoyo unazidi kumhamasisha kutangaza nia na
pindi muda ukifika anaweza kufanya hivyo.
Walibeba na mabango yaliyo na jumbe mbalimbali
Bodaboda nao walifika eneo hilo
Sehemu tu ya umati uliofika nyumbani hapo kwa Lowassa hii leo.
Picha zote kwa hisani ya http://mrokim.blogspot.com/