Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

ANGALIA PICHA- MAGARI HAYA LEO YAMEKABIDHIWA KWA AJILI YA USAFI KATIKA MANISPAA YA SHINYANGA




Hapa ni ofisi za halmashauri ya manispaa ya Shinyanga ambapo leo Jumatatu Machi 16,2015,Kampuni ya uuzaji magari na mitambo nchini Tanzania GF Trucks and Equipment Limited yenye makao yake makuu jijini Dar es salaam imekabidhi magari mawili (Tipper)(PICHANI) kwa halmashauri hiyo yenye thamani ya shilingi milioni 235 yatakayotumika kwa ajili ya usafi katika mji wa Shinyanga pesa zilizotolewa na  benki ya dunia kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali katika halmashauri-Picha zote na Kadama Malunde-Shinyanga
 Mhandisi mwandamizi idara ya Mauzo na Masoko kutoka Kampuni ya uuzaji magari na mitambo nchini Tanzania GF Trucks & Equipment Limited Juma Hamsini( mwenye shati jeupe kushoto) akikabidhi ufunguo wa gari kwa meya wa manispaa ya Shinyanga Gulamhafeez Abubakar Mukadam( katika ofisi za manispaa hiyo.Tukio hilo limeshuhudiwa na madiwani wa manispaa hiyo
Picha ya pamoja wakati wa makabidhiano hayo,wa kwanza kushoto ni Mhandisi mwandamizi idara ya Mauzo na Masoko kutoka Kampuni ya uuzaji magari na mitambo nchini Tanzania GF Trucks & Equipment Limited Juma Hamsini,akifuatiwa na meya wa manispaa ya Shinyanga Gulamhafeez Abubakar Mukadam,wa kwanza kulia ni mratibu wa mradi wa benki ya benki ya dunia(Focal Person) manispaa ya Shinyanga Mwambuli Mwasaga,akifuatiwa na mratibu wa mradi huo Injinia Simon Ngagani

Diwani wa CHADEMA kata ya Kambarage bwana Nyangaka Shilungushela akiwa ameshikilia ufunguo.
Wiki hii pia kampuni hiyo itakabidhi katapila (greda) moja lenye thamani ya shilingi  milioni 520 kwa ajili ya ujenzi wa barabara mbalimbali katika mji wa Shinyanga.

Maneno yanayosomeka katika magari hayo

Magari hayo yenye namba za usajili SM 11328 na SM 11327 yatatumika kwa ajili ya kubebea takataka katika mji wa Shinyanga-Picha zote na Kadama Malunde-ShinyangaBOFYA HAPA UONE KAMPUNI HIYO YA UUZAJI MAGARI NA MITAMBO IKIKABIDHI MSAADA KWA WAHANGA WA MVUA YA AJABU YA MWAKATA KAHAMA


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com