ANGALIA PICHA- LIONS CLUB INTERNATIONAL YATOA MSAADA WA VYAKULA VYA MILIONI 20 KWA WAHANGA WA MVUA KAHAMA


Chama cha Kimataifa kinachotoa misaada mbalimbali ikiwemo ya maafa cha Lions Club International chenye makao yake makuu nchini Marekani leo kimetoa msaada wa chakula wenye thamani ya shilingi milioni 20 kwa wahanga wa mvua katika kijiji cha Mwakata wilayani Kahama mkoani Shinyanga-Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog

Mstahiki meya wa manispaa ya Shinyanga Gulamhafeez Mukadam ambaye ndiyo kafanya kazi kubwa ya kushawishi Lions Club International kutoa msaada huo  akizungumza wakati wa kukabidhi vyakula hivyo kwa uongozi wa Kahama kisha kugawa kwa wahanga wa mvua.

Chama hicho kimegawa kwa kila mhanga wa mvua unga wa sembe  kilo 10,mchele kilo 5,maharage kilo 5,sukari kilo 2,mafuta ya kupikia lita 1,majani ya chai gramu 200,chumvi ½ kilo na maji ya kunywa lita 20 vimegawiwa moja kwa moja wa walengwa badala ya kuacha kwa uongozi husika ikiwa ni utaratibu wa chama hicho kuhakikisha wanawafikia walengwa kama inavyotakiwa.

Wakazi wa Mwakata wakisubiri kupewa msaada na Lions Club International leo


Makamu gavana wa Chama cha Lions Club International katika nchi ya Tanzania na Uganda  Hyderali Gangji akizungumza na akina mama wa Mwakata kabla ya kugawa msaada huo leo 

Kulia ni Makamu gavana wa Chama cha Lions Club katika nchi ya Tanzania na Uganda  Hyderali Gangji akikabidhi unga wa sembe kwa mkuu wa wilaya ya Kahama ndugu Benson Mpesya ambaye amekuwa bega kwa bega na wakazi wa Mwakata tangu kutokea kwa janga la mvua usiku wa kuamkia Machi 4,2015.Wengine wanaoonekana pichani ni wanachama wa Lions Club International ambayo ipo katika nchi 209 duniani
Mkuu wa wilaya ya Kahama akipokea maji ya kunywa

Wanachama wa Lions Club International wakiendelea kukabidhi misaada mbalimbali Mwakata

Wanachama wa Lions Club wakikabidhi mfuko wa mchele wenye kilo 5 ambapo kila mhanga wa mvua alipewa

Mafuta ya kupikia na chumvi vikitolewa

Makamu gavana wa Chama cha Lions Club katika nchi ya Tanzania na Uganda  Hyderali Gangji amesema
chama hicho  kimeguswa na tukio la maafa na kwamba
msaada huo umetokana na mchango wa wanachama wake katika mkoa wa Mwanza ambapo kiasi cha shilingi milioni 20 kimetoka makao makuu ya Lions Club nchini Marekani.

Mkuu wa wilaya ya Kahama Benson Mpesya akizungumza baada ya kupokea msaada huo kutoka chama cha misaada cha kimataifa

 Baada ya kukabidhiana viongozi wa Kahama,meya wa Shinyanga na wanachama wa Lions Club wakapiga picha ya pamoja
Picha ya pamoja

 Lions Club International
BAADA YA KUTOKA KWENYE KAMBI YA WAHANGA,SAFARI KITONGOJI KIMOJA BAADA YA KINGINE KUWAFUATA WAHANGA IKAANZA-Pichani ni gari lililosheheni vyakula 
Hapa ni katika Senta ya Mwakata ambapo ndiyo kilikuwa kituo cha Kwanza kufikiwa na Lions Club leo wakati wa kutoa msaada wa chakula kwa wahanga wa mvua ya mawe na upepo iliyoua watu 46,kuua mifugo na kuharibi vibaya mimea
Hapa ni katika Senta ya Mwakata,
Makamu gavana wa Chama cha Lions Club katika nchi ya Tanzania na Uganda  Hyderali Gangji akiteta jambo na wakazi wa eneo hilo kabla ya kuanza kugawa chakula kwa mtu mmoja baada ya mwingine

Vyakula vikishushwa tayari kwa zoezi la kugawa kwa wahanga wa mvua

 Zoezi la kugawa msaada likaanza kwa kuhakiki kwanza majina ya wanaotakiwa kupatiwa msaada
Mwanachama wa Lions Club akiendelea na zoezi la ugawaji chakula.

Zoezi la ugawaji Linaendelea-kila mhanga wa mvua amepata unga wa sembe  kilo 10,mchele kilo 5,maharage kilo 5,sukari kilo 2,mafuta ya kupikia lita 1,majani ya chai gramu 200,chumvi ½ kilo na maji ya kunywa lita 20
Hapa ni katika kitongoji cha Mbuyuni wakazi wa eneo hilo wakisubiri msaada kutoka Lions Club

 Tunagawa Sisi Wenyewe!!Meya wa manispaa ya Shinyanga Gulamhafeez Mukadam,ambaye ni mwanachama wa Lions Club akihakiki majina ya wahanga wa mvua wanaopaswa kupata msaada katika kitongojo cha Mbuyuni kijiji cha Mwakata
Mwanachama wa Lions Club Nitesh Patel akimpa unga wa sembe mkazi wa Mwakata

Meya wa manispaa ya Shinyanga Gulamhafeez Mukadam,ambaye ni mwanachama wa Lions Club akiwapa pole wakazi wa kitongoji cha  Mwabayanda waliokuwa wamekaa katika shamba la mahindi yaliyoharibiwa vibaya na mvua ya mawe na upepo katika eneo hilo

Zoezi la kushusha chakula likiendelea katika kitongoji cha Mwabayanda katika kijiji cha Mwakata
 Wakazi wa kitongoji cha Mwabayanda katika kijiji cha Mwakata wakiwa katika foleni kuchukua msaada wa chakula kutoka Lions Club


 Akiwa Mwakata meya wa manispaa ya Shinyanga Gulamhafeez Mukadam alikabidhi msaada wa vitu mbalimbali kwa ajili ya wahanga wa mvua katika kijiji cha Mwakata wilayani Kahama uliotolewa na Kampuni ya uuzaji magari na mitambo nchini Tanzania GF Trucks & Equipment Limited yenye makao yake makuu jijini Dar es salaam ambao ni sabuni katoni 20,ndoo 20 za mafuta ya kula na sukari kilo 140 vyote vikiwa na thamani ya shilingi milioni 1.2 -Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post