Rais
Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama salma Kikwete sambamba na viongozi
mbali mbali wa kitaifa wamewaongoza mamia ya waombolezaji kutoa heshima
zao za mwisho kwa mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Mbinga Magharibi Kapteni
John Komba katika Viwanja vya Ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam.
Mwili
wake umepokelewa kwa heshima huku ukiwa umebebwa na Askari maalumu wa
bunge huku ndugu jamaa na marafiki wakiwa katika huzuni ya kuondokewa na
mpendwa wao huyo aliyefariki duniani katika hospitali ya TMJ jijini Dar
es Salaam hapo juzi.
Katika
salamu zake kwaniaba ya kambi Rasmi ya upinzani Mbunge wa Jimbo la
Arumeru Mashariki, Mh.Joshua Nasari ametoa pole kwa marehemu na taifa na
kusema kamba kambi rasmi ya upinzani imeguswa na kifo cha mwanasiasa
mwenzao kwani kila mmoja atarejea na huko ndiko kila mmoja atakwenda kwa
hivyo yatupasa kutengeneza mazingira mazuri kwa familia kwani hakuna
ajuaye siku yake ya mwisho ya kufa.
Amesema
katika kipindi hiki kigumu nidhahiri kwamba kila mmoja anapaswa kusali
na kuomba kwani wao kama kambi rasmi ya upinzani imekuwa nisehemu ya
kuweka siasa mbali na hivyo kuungana na taifa na familia katika kipindi
hiki kigumu.
Rais Kikwete (katikati)
akiwa na makamu wake Gharib Bilal (kushoto) na Anna Makinda katika
viwanja vya Karimjee ili kumuaga marehemu Kapteni John Komba.
Rais Mstaafu Benjamin Mkapa (wa pili kulia) akiwa na mkewe Anna (wa tatu kulia) wakiwasili viwanja vya Karimjee.
Waziri mkuu aliyejiuzulu,Edward Lowassa (kulia)akisalimiana na Mkapa.
Spika wa Bunge, Anna Mkapa (kushoto) akiwa na Mkapa.
Mbunge wa Kinondoni Idd Azzan (kushoto) akiwa na Waziri wa Mambo ya Nje, Bernard Membe.
Aliyekuwa Katibu Mkuu wa CCM, Yusuf Makamba (kulia) akiwa viwanja vya Karimjee.
Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba (kulia)akisalimiana na mwanasiasa mkongwe, Kingunge Ngombale.
Wake wa marehemu Komba, katikati ni mke mkubwa, Salome, na kulia ni mke mdogo.
Miongoni mwa wanafamilia wa marehemu Komba.
~Mpekuzi blog
Social Plugin