Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linamtaka Askofu JOSEPHAT GWAJIMA wa Kanisa la Ufufuo na Uzima afike haraka katika kituo cha Polisi cha Kati ofisi ya Mkuu wa Upelelezi Kanda Maalum ya Dar es Salaam kwa mahojiano kuhusu tuhuma za kashfa na matusi.
"Tumepokea
malalamiko ya kukashifiwa na kutukanwa hadharani Mwadhama Kaldinari
Polycarp Pengo ambaye ni kiongozi wa Kanisa Katoliki nchini Tanzania.
"Kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii kama vile WhatsApp na mingineyo kuna sauti iliyorekodiwa (audio) na picha za video (Video Clip) zikimuonyesha Askofu Gwajima akimkashfu na kumtukana kwa maneno makali Kaldinari Pengo katika hali ambayo pia imewaudhi watu wengine".

Baada
ya tukio hilo juhudi mbalimbali zimekuwa zikifanyika katika hali ya
kawaida ili kumpata Askofu Gwajima bila mafanikio na hivyo yeye mwenyewe
sasa anatakiwa aende akaripoti haraka kwa Mkuu wa Upelelezi wa Kanda
Maalum ya Dar es Salaam bila kukosa.
Ni
muhimu sana kwa Askofu Josephat Gwajima kuripoti yeye mwenyewe badala
ya Kutafutwa au kukamatwa ili ajibu tuhuma hizo kutokana na nafasi yake
katika jamii.
Jalada la uchunguzi limefunguliwa na upelelezi wa shauri hili unaendelea ili sheria ichukue mkondo wake.
Imetolewa na:
S. H. KOVA,KAMISHNA WA POLISI KANDA MAALUM
DAR ES SALAAM
Video Ya Gwajima Akiporomosha maneno mazito.
Social Plugin