Mchungaji
Kiongozi wa Kanisa la Uzima na Ufufuo, Josephat Gwajima amejisalimisha
kituo cha polisi kati kuhojiwa juu ya kutoa lugha chafu dhidi ya Askofu
Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Muadhama Polycarp
Kardinali Pengo.
Mchungaji
Gwajima anadaiwa kumkadhifu na kumtukana hadharani Kardinali Pengo.
Inadaiwa matusi hayo yameonekana kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii
ya WhatsApp na mingineyo, ambapo kuna sauti iliyorekodiwa na picha za
video zikimuonyesha Mchungaji Gwajima akimkashifu na kumtukana kwa
maneno makali Kardinali Pengo katika hali ambayo pia imewaudhi watu
wengine.
Social Plugin