Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

AUAWA KWA KUPIGWA KISHA KUCHOMWA MOTO BAADA YA KUMPASUA KICHWA KWA SULULU MTOTO WA DADA YAKE

 
Mtu moja aliyetambulika kwa jina la YONA MWAMWERE ameteketezwa kwa moto na wananchi wenye hasira kali baada ya kumpasua kichwa mtoto wa dada yake na kufariki dunia papo hapo kwa kutumia sururu  ,ambae alikua akiishi naye maeneo ya Nsalaga Uyole
 
Manati pia zilitumika kumwadhibu


TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI “PRESS RELEASE” TAREHE 16.03.2015.

MTOTO MWENYE UMRI WA MIAKA MITANO AUAWA KWA KUKATWA KICHWA KWA SULULU NA MJOMBA WAKE.

MTOTO MWENYE UMRI WA MIAKA 05 ALIYETAMBULIKA KWA JINA LA JONSON MWAMWERE, MKAZI WA NSALAGA JIJINI MBEYA, ALIUAWA KWA KUPIGWA SULULU KICHWANI  NA KUTENGANISHWA KICHWA NA KIWILIWILI NA  MJOMBA WAKE AITWAYE YONA MWAMWERE (38) MKAZI WA NSALAGA.

TUKIO HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 16.03.2015 MAJIRA YASAA 11:00 ASUBUHI HUKO KATIKA MTAA WA NSALAGA-UYOLE, KATA YA NSALAGA, TARAFA YA IYUNGA, JIJI NA MKOA WA MBEYA.

AWALI INADAIWA KUWA, YONA MWAMWERE ALIKUWA ANAMFUKUZA MTOTO HUYO AMBAYE NI MJOMBA WAKE KUTOKA NYUMBANI NA ALIKIMBILIA KWENYE JENGO LILILOPO JIRANI NA NYUMBANI KWAO AMBALO BADO LIPO KWENYE UJENZI.

HATA HIVYO TAARIFA ZINADAI KUWA, YONA MWAMWEREALIPOFIKA KWENYE JENGO HILO ALIWATISHIA MAFUNDI WALIOKUWA WANAJENGA NA WOTE WALIKIMBIA, HIVYO ALIMUUA MJOMBA WAKE HUYO KWA KUMPIGA KICHWANI KWA SULULU NA KUTENGANISHA KICHWA NA KIWILIWILI.

KUFUATIA TUKIO HILO MAFUNDI WALIOKUWA WAKIENDELEA NA UJENZI WALIPIGA KELELE ZA KUOMBA MSAADA, HIVYO KUNDI LA WANANCHI WALIOAMUA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI WALIJITOKEZA NA KUMSHAMBULIA MTUHUMIWA KWA KUMPIGA HADI KUFA NA KISHA KUUCHOMA MOTO MWILI WAKE.

MAREHEMU WOTE WALIKUWA NI NDUGU WANAOISHI NYUMBA MOJA, MIILI YAO IMEHIFADHIWA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA. CHANZO CHA TUKIO HILI KINACHUNGUZWA INGAWA UCHUNGUZI WA AWALI UNAONYESHA KUWA MAREHEMU YONA MWAMWEREALIKUWA NA MATATIZO YA AKILI.

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA POLE KWA FAMILIA YA MAREHEMU KUTOKANA NA TUKIO HILO. AIDHA ANATOA WITO KWA JAMII/WANANCHI KUACHA TABIA YA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA BADALA YAKE WAJENGE TABIA YA KUWAFIKISHA KATIKA MAMLAKA HUSIKA WATUHUMIWA WANAOWAKAMATA KWA TUHUMA MBALIMBALI KWA HATUA ZAIDI ZA KISHERIA.

Imesainiwa na:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com