Mbunge
wa Jimbo la Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe jana March 14 ametoa gari
mpya ya kubebea wagonjwa (Ambulance)kama moja ya ahadi zake alipokuwa
kwenye kampeni ambapo aliahidi kabla ya kumaliza kipindi cha uongozi
wake atatoa gari hiyo.
Wananchi wakipokea
msaada huo Michael Mwandezi ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa
halmashauri ya Kigoma pamoja na Hamis Said Betese ambaye naye ni
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma ambapo kwa niaba ya
wananchi wa kata ya Nyarubanda ambao ndio msaada huo wamemshukuru sana
Mbunge Zitto Kabwe.
Hata
hivyo kabla ya kuelekea kukabidhi Gari hiyo ya kubebea wagonjwa,Zitto
Kabwe aliwatembelea Wanachama wa Chama cha Ushirika Rumaco ambao
wanajishughulisha na kilimo cha Kahawa kutoka kijiji cha Matyazo Kigoma
Kaskazini.
Hapa Zitto akiwa kwenye shamba lake la kahawa
Social Plugin