Mchezaji
mganda alieleta vuta nikuvute kati ya Klabu Vigogo Nchini baada ya
kuhama kwenda nyingine kwa mizengwe mikubwa, Emmanuel Okwi, Leo hii
alileta raha kubwa kwa Simba baada ya kufunga Bao pekee na la ushindi
walipoilaza Yanga Bao 1-0 kwenye Mechi ya Ligi Kuu Vodacom.
Bao
hilo la Okwi lilifungwa Dakika ya 53 na kuipandisha Simba hadi Nafasi
ya 3 wakiwa na Pointi 26 kwa Mechi 17 na juu yao wapo Mabingwa Watetezi
Azam FC wenye Pointi 30 kwa Mechi 16 na Yanga bado wapo kileleni wakiwa
na Pointi 31 kwa Mechi 16.
Yanga walimaliza Mechi hii wakibaki Mtu 10 baada ya Mchezaji wao Haruna Niyonzima kutolewa nje kwa Kadi Nyekundu karibuni na mwisho.
MATOKEO- Mechi zilizopita:
Jumamosi Machi 7
Coastal Union 2 Kagera Sugar 2
JKT Ruvu 0 Azam FC 1
Social Plugin