Nyumba ya Robinson Massawe(picha kutoka maktaba ya Malunde1 blog) |
Robinson Massawe enzi za uhai wake |
Habari za kusikitisha kutoka Shinyanga ni kwamba Robinson Massawe mkazi wa Bushushu kata ya Lubaga mjini Shinyanga amefariki dunia baada ya gari aina ya Noah aliyokuwa anaendesha kuacha njia na kugonga mti katika eneo la Samuye barabara ya Tinde Shinyanga.
Robinson ndiye siku takribani 20 zilizopita , nyumbani kwake
binti anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 23- 25
anayedaiwa kuwa ni mchawi alikutwa amenasa kwenye mlango wa nyumba yake huku akiwa amevaa kishirikina na mwili
wake ukiwa umepakwa dawa nyeusi akidai alikuwa anaongoza wenzake zaidi ya 10
kutoka kanda ya ziwa kuwanga katika nyumba hiyo.
Mtandao huu wa Malunde1 blog umeambiwa kuwa ajali hiyo iliyosababisha vifo vya watu wawili imetokea jana majira ya saa 12 jioni wakati akielekea Busanda na mwenzake aliyejulikana kwa jina la Jacob mkazi wa Majengo mjini Shinyanga,ambaye ni fundi umeme,ambaye pia alifariki katika ajali hiyo.
Chanzo cha ajali hiyo kinatajwa kuwa mwendokasi na kutumia pombe kupindukia.
Tukio hilo limezua gumzo huku likihusishwa na imani za kishirikina kwani mwili marehemu Robinson umekutwa na kovu kidogo usoni na kwamba ni wiki chache mtu anayedaiwa kuwa mchawi alinasa katika nyumba yake.
Habari zilizotufikia zinasema kuwa kabla ya kifo chake hata nyumbani kwake kulikuwa na vitendo vya mauza uza.
Katika tukio la binti aliyedaiwa kuwa mchawi lilitokea Februari 13 mwaka huu,mashuhuda wa tukio walisema baada ya kumhoji binti huyo alisema alifika kwenye familia hiyo,akiwa kiongozi wa kundi la wachawi zaidi ya 10 kutoka Ushirombo,Misungwi na Shinyanga saa 9 usiku kwa ajili ya kufanya sherehe baada ya kufanikiwa kusambaratisha kichawi ndoa ya Massawe na Mary Joseph.
Siku ya tukio la binti huyo anayedaiwa kuwa mchawi,Askari Polisi akimwokoa binti huyo nje ya nyumba ya bwana Robinson Massawe(picha kutoka maktaba ya Malunde1 blog)
BONYEZA MANENO HAYA KUONA PICHA ZAIDI ZA BINTI HUYO
Mungu ailaze mahali pema peponi roho ya marehemu Robinson Massawe,Malunde1 blog inawapa pole ndugu,jamaa na marafiki waliofikwa na msiba huu