Watu
wawili wamefariki dunia papo hapo na wengine watatu kujerihiwa baada ya
basi la FM safari likitokea Dar es Salaam kwenda mkoani Mbeya kugongana
uso kwa uso na fuso iliyo sheheni nyanya katika eneo la hifadhi ya
mikumi barabara ya Morogoro Iringa.
Wakizungumza
nasi mashuhuda wa ajali hiyo wamesema chanzo cha ajali hiyo ni dereva
wa basi kutaka kulipita gari lingine na hivyo kugongana usokwa uso
ambapo wametupia lawama baadhi ya abiria kuwachochea madereva kuendesha
kasi na ambapo wameshauri vyombo vya usalama barabarani kuwachukulia
hatua madereva wazembe wanaosababisha vifo visivyo vya lazima.
Kamanda
wa polisi mkoa wa Morogoro Leonard Paulo amewataja walio fariki katika
tukio hilo kuwa ni Seth Mapunda ambaye ni dereva wa fuso na mwanamke
mmoja ambaye hajafahamika majina yake na jeshi la polisi linamshikilia
dereva wa basi kwa kusababisha ajali.
Watu
wawili wamefariki katika ajali iliyotokea huko Mikumi kati ya basi
lenye namba za usajili T 179CRG mali ya Fm safari linalotoka Dar es Salaam kwenda Mbeya kugongana lori aina ya Fuso.
Baadhi ya wasamaria wema wakiendelea kuokoa abiria waliokuwa kwenye basi hilo lililopata ajali maeneo ya Mikumi mkoani Morogoro.
Hii ndio hali halisi ya magari baada ya kupata ajali eneo la Mikumi
|
eneo la tukio