Basi la Mantale Tours likiwa eneo la tukio-Picha na Richard
Kabega-Malunde1 blog Shinyanga
Watu wawili wanadaiwa kufariki dunia katika ajali
iliyohusisha gari dogo aina ya Noah na basi la Mantale Tours likitoka Mwanza
kwenda Kahama katika eneo la Kituli barabara ya Tinde Kahama mkoani Shinyanga.
Ajali hiyo imetokea jana saa tatu usiku ikihusisha basi hilo
linalofanya safari zake Mwanza Kahama na gari hiyo ndogo inayofanya safari zake
Didia hadi Shinyanga mjini.
Mmoja wa mashuhuda wa ajali hiypo Robert Njile Monday
ameiambia Malunde1 blog kuwa dereva wa gari ndogo anayejulikana kwa jina
la Chomola aliyefariki papo hapo alikuwa katika
mwendokasi na kusababisha ajali hiyo.
Amesema kutokana na mwendokasi huo aligonga bams iliyopo
katika eneo la barabara ya kwenda Shule ya sekondarii Kituli gari ikamshinda na
hatimaye kugongana na basi hilo.
Habari kutoka eneo la tukio zinasema kuwa gari ndogo ilikuwa
na dereva na abiri mmoja anayedaiwa kufariki pia ambapo dereva wa basi aliumia
kidogo na abiria wake
Social Plugin