Habari tulizozipata hivi punde kutoka Nzega ni kwamba magari matatu yamegongana muda mfupi uliopita. Malunde1 blog imeambiwa kuwa kati ya magari hayo limo basi lililokuwa linatokea Mbeya kwenda Mwanza,lori ,landcruiser inayodaiwa kuwa ni ya serikali na yamegongana eneo la Nzega ndogo mkoani Tabora. Chanzo cha ajali ni gari aina ya Landcruiser inayodaiwa, ilikuwa katika mwendo kasi. Habari za awali zinasema kuwa gari hiyo aina ya landcruiser ilikuwa imebeba watumishi wa halmashauri ya Nzega waliokuwa wanatokea kwenye ukaguzi na maafisa wa TFDA na watu watano waliokuwa katika gari hilo wanadaiwa kupoteza maisha. SOMA HABARI KAMILI HAPA |
Social Plugin