TUNDU LISSU ATANGAZA RASMI :ZITTO SIO MWANACHAMA TENA WA CHADEMA!!

  
Mwanasheria mkuu wa chama cha upinzani nchini CHADEMA, Tundu Lissu leo ametangaza kuvuliwa uanachama kwa mbunge wa Kigoma Kasikani Zitto Kabwe baada ya Mahakama Kuu ya Tanzania kanda ya Dar es Salaam kutupilia mbali pingamizi la mbunge huyo la kuzuia asijadiliwe.


"Kwa mujibu wa katiba ya chama cha CHADEMA, mwanachama yoyote anapofungua kesi mahakamani dhidi ya chama chake, endapo atashindwa katika kesi hiyo atakuwa amejiondoa uanachama wake, kwahiyo natangaza rasmi rasmi Zitto Kabwe sio mwanachama tena wa Chadema. 

Kwa upande wake Zitto Kabwe amesema hawakuwa na wito wa mahakamani leo na Jaji wa kesi kahamishiwa Tabora na hawana taarifa ya Jaji Mpya, pia kaongeza kuwa Mwanasheria anafuatilia na atatoa statement.

Licha ya kutupilia mbali kesi ya Mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe, Mahakama kuu imemtaka kulipa gharama zote za kesi toka ilivyoanza.

Mwaka jana Zitto Kabwe aliweka pingamizi mahakamni kuzuia kikao cha Kamati Kuu kumjadili na hoja yake ilikuwa ni kupinga kuitisha kamati kuu kabla shauri lake kusikilizwa na Baraza Kuu.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post