Abiria wanaokwenda mikoa
ya Mwanza, Singida na Dar es salaam na Kwingineko na wale wanaokwenda
mikoa ya Kigoma na magari yote yanayokwenda nchi jirani za Rwanda,
Burundi, Uganda na Congo, wamekwama baada ya wananchi wa kijiji cha
Mwakata Kata ya Isaka wilayani Kahama kufunga barabara kuu ya kwenda
maeneo hayo asubuhi hii.
Taarifa kutoka eneo la tukio zinasema kuwa wahanga hao wa janga la mvua ya mawe na upepo iliyoua watu 46 na
kujeruhi wengine zaidi ya 90, wameifunga barabara hiyo kuishinikiza
serikali kuwapa misaada ya chakula na malazi.
Inaelezwa kuwa misaada ambayo imetolewa katika maeneo mbalimbali na kwamba serikali ya eneo hilo haijagawanya wahanga wanaohusika badala yake kupewa watu wengine.
Inaelezwa kuwa misaada ambayo imetolewa katika maeneo mbalimbali na kwamba serikali ya eneo hilo haijagawanya wahanga wanaohusika badala yake kupewa watu wengine.
Mpaka sasa mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ya Kahama ambaye pia
ni mkuu wa wilaya hiyo Benson Mpesya ameshaenda eneo la tukio ili
kuwasikiliza wananchi hao na kujaribu kumaliza tatizo hilo.
Hata hivyo habari
tulizozipata hivi punde zinasema kuwa tayari jeshi la polisi wilaya ya
Kahama limefika katika eneo la tukio na kutumia mabomu ya machozi bila
kuathiri wananchi na kufanikiwa kuwatawanya na kufungua barabara ambapo
tayari magari yameanza kupita.
Ikumbukwe kuwa juzi Alhamisi Waziri mkuu Mizengo Pinda alikwenda kuzuru eneo hilo lililokumbwa
na maafa hayo kwa ajili ya kutolewa kwa misaada ya kibinadamu, ambapo
pia mazao shambani na vyakula vilivyokuwa majumbani pamoja na mifugo
vimeathiriwa.
Tukio la kufungwa kwa barabara limekuja siku moja tu baada
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi mkoa wa Shinyanga Khamis Mgeja kuibuka na kudai kusikitishwa na utendaji kazi wa mkuu wa wilaya ya Kahama Benson Mpesya kwa kushindwa kusimamia kikamilifu kamati ya ugawaji chakula na vifaa hali iliyosababisha waathirika wa mvua ya mawe na upepo katika kijiji cha Mwakata wilayani Kahama,kugombea chakula na kulalamikia kuuzwa kwa magodoro na branketi zilizotolewa misaada na wahisani.
ANGALIA PICHA ZAIDI LA TUKIO LA WANANCHI KUFUNGA BARABARA HAPA

Hayo yamejiri Jana Ijumaa wakati kamati ya maafa ya mkoa ikipokea misaada
kutoka taasisi mbalimbali za fedha, mashirika na watu binafsi walioguswa
na kutoa misaada ya chakula, magodoro na nguo.
Mwenyekiti wa CCM
mkoa wa Shinyanga Khamis Mgeja alisema kuwa endapo utendaji wa wakuu
wa wilaya kama alivyo mkuu wa wilaya ya Kahama usipobadilika Chama Cha Mapinduzi kitapata wakati mgumu katika
uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 kwa kuwa baadhi yao hawaendani na sera ya
chama.
Akijibu tuhuma hizo mkuu wa wilaya ya Kahama Benson Mpesya
alisema kuwa yeye hausiki na upotevu wa vifaa vinavyodaiwa kuibiwa na
kuuzwa kwa watu wasiohusika na kusema kwamba rawama hizo zielekezwe
kwenye kamati ya maafa ya ugawaji.
Kufuatia hali hiyo mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ally Nasoro Rufunga
alilazimika kuingilia kati mgogoro huo na kuwaita wote kwa pamoja katika
kikao cha zarula ambapo hakutaka kubainisha hatua zilizochukuliwa na
kusema kwamba serikali imepokea maagizo ya kiongozi wa chama cha
mapinduzi na kuyafanyia kazi kwa lengo la kuhakikisha waathirika
wanapata huduma inayositahili.
ANGALIA PICHA ZAIDI LA TUKIO LA WANANCHI KUFUNGA BARABARA HAPA
Social Plugin