Harusi moja imetibuka nchini India baada ya bwana harusi kufeli swali rahisi sana la hisabati aliloulizwa na bi harusi.
Kulingana na ripoti za walioshuhudia kioja hicho cha aibu bi harusi anasemekana alimuuliza bwana harusi
''15 ukiongeza 6 utapata nini ''?
Polisi
katika jimbo la Uttar Pradesh nchini India wanasema kuwa sherehe za
harusi hiyo zilitibuka baada ya bi harusi kufoka mumewe mtarajiwa
alipotoa jibu lake ni ''17 ''
Alikurupuka na kuondoka jukwaani akiwa amenuna akisema hawezi kuoa mtu ambaye hakwenda shuleni.
Juhudi zote za jamaa na marafiki waliofika kushuhudia sherehe hiyo ziliambulia patupu.
Polisi
katika jimbo hilo la Uttar Pradesh wanasema kuwa jamaa wa bwana na bi
harusi wote walikubaliana kurejesheana zawadi zote walizokuwa wametoa
kwa ajili ya wapendwa hao.
Asilimia kubwa ya ndoa zote nchini India
hupangwa na wazazi na mara nyingi maharusi hukutana kwa mara ya kwanza
katika sherehe za harusi yao.
Babake bi harusi Mohar Singh aliyekuwa amepanga harusi hiyo katika
kijiji cha Rasoolabad aliiambia idhaa ya kihindi ya BBC kuwa mwanawe
alishangaa kuwa mumewe mtarajiwa Ram Baran hakuwa msomi.
Mwezi
uliopita bi harusi mwengine aliolewa na mgeni katika harusi yake baada
ya Mumewe aliyekuwa amepanga kumuoa kuanguka kifaa dakika chache tu
kabla ya wawili hao kuunganishwa kuwa mume na mke .
via>>BBC
via>>BBC
Social Plugin