"...
Chama ambacho kimejengwa katika misingi ya ubaguzi na damu ya
watanzania hakiwezi kudumu, kitakufa tu....ndio Kinakufa na
wasituhusishe na kifo chao, wanakufa kwa Ujinga wao wenyewe..."
Nape Moses Nnauye - Katibu wa Uenezi na Itikadi wa Chama Cha Mapinduzi.
Mkutano wa hadhara Mto wa Mbu, Monduli.
Tarehe 13th March 2015.
Ni siku mbili tu baada ya maneno hayo ya Nape, Nyumba ya jirani
ameshatua Bundi, tena ametua kwenye kiunga cha Nyumba hiyo, Mkoani
Arusha.
Ambapo aliyekuwa Mwenyekiti wa CHADEMA wilaya ya Ngorongoro
ndugu Revocatus William Parapara amejiondoa kwenye Chama hicho na
kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM), Ndugu Parapara amefanya maamuzi
hayo jioni ya leo katika mkutano wa hadhara, eneo la Wasso, Loliondo ambao
umehutubiwa na Ndugu Abdulrahman Kinana-Katibu Mkuu wa CCM ambae
anaendelea na ziara yake katika Mkoa wa Arusha.
Ndugu Revocatus Parapara mekuwa Kiongozi Mwandamizi wa Chadema katika
wilya ya ngorongoro kwa Miaka zaidi ya 10. Na katika mkutano huo ndugu
Parapara amesema hawezi kuendelea kushiriki kupanda mbegu ya ubaguzi
ambayo inaendelea kumea katika Chama Chake cha zamani cha CHADEMA.
Aidha aliyekuwa Makamo Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake CHADEMA
(BAWACHA) Bi. Elinami Limbali amekihama Chama hicho akiongozana na
Mwenyekiti wake wa Wilaya na Kujiunga na Chama Cha Mapinduzi, akidai
kuchoshwa na sera za kuhamasisha vurugu badala ya maendeleo zinazofanywa
na CHADEMA, na kusema kuwa zinapotokea vurugu watoto na akina mama ndio
hupata tabu.
via>>Jamii Forums