SIKU
mbili baada ya kuwachiwa mtuhumiwa Khalid Kagenzi anayedaiwa kutaka
kumuua kwa sumu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo
(Chadema), hatimaye Katibu Mkuu wa chama hicho Dk. Willibrod Slaa, naye
amehojiwa leo.
Dk. Slaa alifika Kituo Kikuu cha Kati majira ya saa nne asubuhi kwa ajili yakuhojiwa na kuandika maelezo kuhusu tukio la kutaka kuuawa kwa kulishwa sumu.
Katika mahojiano hayo, Dk. Slaa aliongozana na wanasheria wake Nyoronyo Kicheere na John Malya, yalichukua muda wa saa sita huku baadhi ya wananchama waliombatana naye wakimsubiri nje.
Baadhi ya viongozi aliyoongozana nao walikuwa ni Profesa Abdallah Safari ambaye ni makamu mwenyekiti wa chama hicho Bara, Godbles Lema na John Heche.
Akizungumza na wandishi wa habari mara baada ya kumaliza mahojiano hayo, Dk Slaa, alisema kuwa maelezo hayo yatumika katika ushahidi kuhusu tukio hilo.
Aidha Diwani Ubungo (Chadema), Jacob Boniface, alikuwa akihojiwa hata hivyo hadi waandishi wanaondoka katika eneo hilo alikuwa hajotoka kituoni hapo.
Kufikishwa katika kituo hicho kumetokana na sakata Chadema kutoa taarifa kwenye vyombo vya habari kwamba kulikuwa na mpango wa mlinzi wake Kagenzi kutaka kumuua kwa sumu.

Social Plugin