DR SLAA AHOJIWA NA POLISI KWA SAA SITA KUHUSU TUHUMA ZA KUTAKA KUWEKEWA SUMU NA MLINZI WAKE

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhXCcP4V-gykCkZJpZCODILD1pxX2aJByRp5b8AtvFRCOs5yzzyyTpEd4YgETqfcDdOp4aXCZuQaasjQEhyxD-DI1lX9cMOnWgRH1_P45-aR69yyhptpvzXm0rYZ1Cs4dddwvMh5ekLJiNP/s1600/Slaa+akitoka+Pols.JPG
Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Willibrod Slaa (kulia) akitoka Kituo Kikuu cha Polisi jijini Dar es Salaam leo huku akiambatana na wanasheria wake, John Mallya (kushoto) na Nyaronyo Kicheere ambapo aliandika maelezo na kuhojiwa na Polisi kwa saa sita kuhusiana na tuhuma za kutaka kuuwawa na mlinzi wake, Khalid Kagenzi. (Picha na Francis Dande)

SIKU mbili baada ya kuwachiwa mtuhumiwa Khalid Kagenzi anayedaiwa kutaka kumuua kwa sumu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), hatimaye Katibu Mkuu wa chama hicho Dk. Willibrod Slaa, naye amehojiwa leo.

Dk. Slaa alifika Kituo Kikuu cha Kati majira ya saa nne asubuhi kwa ajili yakuhojiwa na kuandika maelezo kuhusu tukio la kutaka kuuawa kwa kulishwa sumu.

Katika mahojiano hayo, Dk. Slaa aliongozana na wanasheria wake Nyoronyo Kicheere na John Malya, yalichukua muda wa saa sita huku baadhi ya wananchama waliombatana naye wakimsubiri nje.

Baadhi ya viongozi aliyoongozana nao walikuwa ni Profesa Abdallah Safari ambaye ni makamu mwenyekiti wa chama hicho Bara, Godbles Lema na John Heche.

Akizungumza na wandishi wa habari mara baada ya kumaliza mahojiano hayo, Dk Slaa, alisema kuwa maelezo hayo yatumika katika ushahidi kuhusu tukio hilo.

Aidha Diwani Ubungo (Chadema), Jacob Boniface, alikuwa akihojiwa hata hivyo hadi waandishi wanaondoka katika eneo hilo alikuwa hajotoka kituoni hapo.

Kufikishwa katika kituo hicho kumetokana na sakata Chadema kutoa taarifa kwenye vyombo vya habari kwamba kulikuwa na mpango wa mlinzi wake Kagenzi kutaka kumuua kwa sumu.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
أحدث أقدم