Mwanaume mmoja Nigeria Udeme Inim amekamatwa kwa madai ya kumshambulia na kumng’ata sikio mtoto wake wa kiume wakati akiamulia ugomvi kati yake na mke wake nyumbani kwao mtaa wa Asaka, Nigeria.
Kulitokea hali ya kutokuelewana kati ya wawili hao, Inim alianza kumpiga mke wake ndipo kijana huyo Christopher Bassey alipoingilia kwa lengo na kumwokoa mama yake lakini baba yake alipatwa hasira na kumng’ata sikio na kulikata.
Bassey
alipelekwa Hospitali ya jirani lakini madaktari hawakufanikiwa
kurudishia sikio hilo, mwanaume huyo alikamatwa na kushtakiwa kwa kosa
la kushambulia na kuwekwa jela huku dhamana yake ikiwa ni Naira
20,000.
Social Plugin