Picha behind the Scene katika filamu ya "Firigisi" inayohusu ukatili dhidi ya watu wenye albinism. |
Madini yanayotajwa kuwa na uhusiano na vitendo vya ukatili kwa watu wenye ulemavu wa ngozi
Picha behind the Scene Filamu hiyo
Picha Behind the Scene |
Filamu ya kusisimua inayohusu ukatili wa watu wenye ulemavu
wa ngozi(Albino) inatarajia kuzinduliwa mwezi April Mwaka huu.Filamu hiyo
iliyopewa jina la “FIRIGISI” imefanywa na wasanii kutoka mkoa wa Shinyanga(
Bongo Movie Shinyanga) na msanii Dennis Sweya maarufu Dino kutoka Bongo Movie
Dar es salaam.
Dino ameigiza na kuongoza Filamu hiyo ambayo imebeba maudhui
kuhusu Ukatili wanaofanyiwa watu wenye Albinism nchini Tanzania huku watu
mbalimbali wakitajwa kuhusika katika ukatili huo wakiwemo
wafanyabiashara,wachimbaji wa madini na wanasiasa.
Akizungumza na Malunde1 blog mjini Shinyanga Mwongozaji wa
Filamu hiyo Dennis Sweya( Dino) amesema filamu hiyo ina maudhui mazuri kwani
hata mazingira yake ni ya Kanda ya Ziwa ambako ndiko vitendo hivyo vya ukatili
vimekuwa vikifanyika.
“Ni filamu ya kiwango cha juu sana inasisimua,imeandaliwa na
wasanii kutoka mkoa wa Shinyanga,msanii
pekee kutoka Dar es salaam ni mimi ambaye nimeigiza na Kuongoza Filamu
hii,production yake pia imefanyika Dar es saalam kwani wapiga picha wanatoka
Dar es salaam ambao ni Amani Masuka akishirikiana na Benny Luoga”,ameeleza
Dino.
“Filamu hii ina maudhui yanayogusa Kanda ya Ziwa kwani ndiyo
inaonekana kuwa ina matatizo makubwa ya ukatili wa watu wenye albinism,tumejitahidi
kuielimisha jamii,tumeonesha,chanzo cha vitendo hivyo, kipi wanapaswa
wajue,nini kifanyike,nini kinawaponza na mambo kadha wa kadha”,ameongeza Dino.
Dino amesema washiriki katika filamu hiyo ni watu wanayoyajua
vyema mazingira ya Kanda ya ziwa na kwamba miongoni mwa wahusika wakuu yumo
kijana mwenye Albinism hali ambayo imefanya filamu hiyo iwe katika kiwango cha
juu na wanategemea filamu hiyo itakuwa katika kiwango cha Kimataifa kwani
haijawahi kutokea.
Amesema mdhamini mkuu aliyetoa mamilioni ya fedha
kufanikisha kutengenezwa kwa katika
filamu hiyo ni ndugu Willy Mzava wa mjini Shinyanga na kwamba filamu hiyo
inatarajia kuzinduliwa mjini Shinyanga kati ya Mwezi Aprili na Mei mwaka huu
huku wageni wakiwemo wafanyabiashara wakitarajiwa kuhudhuria uzinduzi huo
ambapo mgeni rasmi atakuwa mtu mkubwa sana hapa nchini ingawa hakutaka kutaja
jina lake.
Aidha Dino amesema kauli mbiu waliyotumia katika filamu hiyo
ni “Albino ni Mimi na
Wewe,Tuwalinde,Tuwapende na Tuwathamini(TTT)” ikiwa ina maanisha kuwa kibaiolojia
mwanamme na mwanamke mweusi wanaweza kukutana na kuzaa mtoto mwenye Albinism,na
kwamba ni ndugu zetu Tunazaa wenyewe kwani huwezi jua kesho kitatokea nini,mtu
yeyote anaweza kuzaa mtoto mwenye albinism.
Mwenyekiti wa Bongo Movie Shinyanga Juma Ibrahim Songoro (Songoro
Gaddafi) amewaomba wakazi wa Shinyanga,kanda ya ziwa na nchi kwa ujumla kuunga
mkono kazi yao ya kwanza na kuahidi filamu hiyo kuzinduliwa haraka iwezekavyo.
“Hii ni filamu ya aina yake,haijawahi kufanywa popote
duniani,hatujaiga mahali popote kama wanavyofanya baadhi ya wasanii,na filamu
hii ina mvuto,inasikitisha,inasisimua,inafunza,inaonya,inaelimisha
kwa kila mtu atakayeiangalia hivyo tunaamini itapokelewa siyo tu kitaifa bali
kimataifa”amesema Songoro
Na Kadama Malunde-Shinyanga
MSIKILIZE HAPA CHINI DIRECTOR WA FILAMU YA FIRIGISI DENNIS SWEYA( DINO) AKIZUNGUMZIA FILAMU HIYO