Treni
ambayo ilikuwa na kichwa kimoja ikielekea kuchukua mabehewa asubuhi ya
leo imegongwa na gari kubwa la mizigo eneo la Karume jijini Dar na
kusababisha foleni ndefu eneo hilo.
Tukio
hilo limejiri asubuhi ya saa 12 alfajiri ambapo gari hilo lilikuwa
likipita kwa kasi bila kufuata alama za barabarani zinazoonesha sehemu
ya reli.
Akizungumza
na mwandishi wetu, Ofisa Oparesheni Shirika la Reli, Mohamed Kanka,
alisema kuwa treni hiyo ilikuwa ikipita majira ya saa kumi na mbili
alfajiri na kugongwa na gari iliyokuwa ikipita pasipo dereva wa gari
hiyo kuzingatia alama iliyokuwa ikionesha kama sehemu hiyo kuna reli.
Alisema
kuwa katika ajali hiyo dereva wa gari na dereva aliyekuwa katika treni
hiyo wameumia na wamekimbizwa Hospitali ya Amana Ilala kwa ajili ya
kupatiwa matibabu.
Vilevile
alisema baada ya ajali hiyo kutokea gari jingine lililokuwa limesimama
liligongwa na kichwa cha treni baada ya kuiacha njia yake na kuelekea
upande wa magari yaliyokuwa yakipita.
Social Plugin