Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

WALIOFARIKI AJALI YA BASI HUKO IRINGA SASA 42,MAJERUHI WENGI ,9 HALI ZAO NI MBAYA




Habari kutoka Iringa zinasema kuwa idadi ya watu waliofariki dunia katika ajali ya basi la Majinja Express ambalo lililokuwa likitokea Mbeya kwenda Dar es Salaam kufunikwa na kontena maeneo ya Changalawe, Mafinga mkoani Iringa,hadi saa 10 jioni ni watu 42 wamefariki dunia.


Chanzo cha habari cha Malunde1 blog kinasema kuwa  hadi muda huo majeruhi walikuwa 22 na mtoto mmoja mwenye umri wa miaka 4 kati ya abiria waliokuwa katika basi hilo hajaumia hata kidogo.

Habari kutoka  katika hospitali ya Mafinga ni kwamba majeruhi 9 hali zao ni mbaya.

Kwa mujibu wa mashuhuda wa ajali hiyo ni kwamba dereva wa basi alikuwa akijaribu kulipita lori ndipo walipodondokewa na kontena hilo.
BONYEZA MANENO HAYA KUSOMA HABARI KAMILI,KUJUA MAJINA YA ABIRIA WALIOKUWA KATIKA BASI HILO NA KUONA PICHA ZAIDI YA 20 ZA TUKIO HILO LA KUSIKITISHA 

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com