Watu wengi wamekuwa wakilalamikia teknolojia na ufundi wa simu nyingi za kisasa wengi wakiwaponda wabunifu kwa misingi ya kuwaasilimia kubwa ya simu za mfumo wa 3G na zaidi zinatengezwa kwa plastiki.
Sasa basi,bwana mmoja mbunifu amekuja na jibu ya kutengeza simu kutokana na ''Nyasi'' .
Bwana Sean Miles amezindua simu itakayokuwa ya kipekee.
Simu hiyo ndiyo ya kwanza kuwahi kutengenezwa kwa asilimia 100% kutokana na bidhaa hii.
Gamba la juu la simu hiyo limeundwa kwa bidhaa inayotokana na nyasi
maalum iliyochanganywa na kemikali fulani na kiungo (resin)
"mchanganyiko huu maalum unatoa sura kama vile (carbon) alisema Miles.
Mfumo huo unachanganywa na kumbwa kwa njia itakayoruhusu watengezaji wa simu kuumba gamba la simu inayotokana na nyasi.
Bwana Miles alikuwa amepewa kandarasi na kampuni ya simu ya O2
kutafuta mbinu ya kutumia upya bidhaa ambazo zimekosa wateja ama
zimezeeka.
Hata hivyo kitengo cha ubunifu kilitamaushwa na ubunifu
wake na sasa kimeanza mikakati ya kutathmini uwezo wa kampuni hiyo
kuunda kwa wingi magamba ya simu.
Kufikia sasa asilimia 25% ya simu nzee nchini uingereza zinarekebishwa na kutumiwa upya.
Via>>BBC
Via>>BBC
Social Plugin