Hakimu
wa Mahakama ya Mwanzo ya Somanda Wilayani
Bariadi Janeth Mazigi(28) amefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Bariadi kwa makosa manne(4) aliyoyatenda dhidi ya mtumishi wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi kwa kile kinachosadikiwa kuwa ni wivu wa mapenzi akimtuhumu kutembea na mme wake.
Bariadi Janeth Mazigi(28) amefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Bariadi kwa makosa manne(4) aliyoyatenda dhidi ya mtumishi wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi kwa kile kinachosadikiwa kuwa ni wivu wa mapenzi akimtuhumu kutembea na mme wake.
Hakimu
huyo inadaiwa kuwa alitumia wadhifa alionao kumteka mtumishi huyo (jina linahifadhiwa) na kumnyanyasa
kijinsia kinyume na sheria ya kanuni ya Adhabu sura ya 16.
Akisomewa
mashtaka hayo na Wakili wa Serikali Mfawidhi Mkoani Simiyu Yamiko Mlekano mbele
ya hakimu Mfawithi mahakama ya wilaya
Bariadi Aidan Mwilapwa wakili huyo alisema kuwa mshitakiwa anatuhumiwa
kwa kosa la wizi, utekeji, unyanyasaji, pamoja na kukutwa na picha utupu.
Mlekano
aliieleza mahakama kuwa mnamo tarehe 3/03/2015 mshtakiwa pamoja na askati polisi wa kike
walimteka Mtumishi huyo ofisini kwake kinyume na matakwa yake na kumpeleka
nyumbani kwa mshitakiwa Kidinda Bariadi Mjini kinyume na kifungu namba 133 cha
kanuni ya adhabu sura ya 16.
Kosa
la pili la unyanyasaji wa kijinsia , ilidaiwa kuwa katika tarehe hiyo hiyo
majira ya saa 3 asubuhi nyumbani kwa Mshtakiwa , alimpiga picha za utupu
mtumishi huyo kwa kutumia simu yake kwa lengo la kumdhalilisha na kumtolea maneno
ya kashfa.
Kosa
la tatu ni ,kukutwa na picha za uzalilishaji mshitakiwa ilidaiwa terehe hiyo hiyo majira
ya saa 3 asubuhi nyumbani kwa mshitakiwa alikutwa na picha za utupu zilizokuwa
katika simu yake alizokuwa amempiga mtumishi huyo akiwa uchi kwa lengo za kuzituma katika mitandao ya kijamii
ili kumdhalilisha kinyume na sheria na kanuni ya adhabu.
Kosa
la nne ambalo ni wizi ilidaiwa mshitakiwa alimnyang'anya Mtumishi huyo kiasi cha
pesa taslimu Tsh 50,000, power bank, chaji, airphone, simu mbili za aina ya Son
na Tecno vyote hivyo vikiwa na thamani ya Sh Mil 1,405,000.
Hata
hivyo mshitakiwa alikana makosa hayo, ambapo aliachiwa huru kwa baada ya kupata
dhamana, huku hakimu wa mahakama hiyo akiahirisha kesi hadi mnamo tarehe 2/04/2015.
Hata
hivyo mshitakiwa huyo wakati anatenda makosa hayo alishirikiana na askari
polisi kituo cha polisi Bariadi, ambaye hakuweza kupatikana jina lake, huku
taarifa zikisema kuwa askari huyo bado anashughulikiwa na mamlaka zilizoko chini
yake kijeshi.
Mshtakiwa
anadaiwa kutenda makosa hayo nyumbani kwake huko Kidinda na
kwamba chanzo kinasadikiwa ni wivu wa
mapenzi ambao ulipelekea kumtuhumu Mtumishi huyo kuwa anatembea na mume wake.
Via>>http://simiyunews.blogspot.com/
Via>>http://simiyunews.blogspot.com/