DUNIA
haikaukiwi matukio ya kustaajabisha, kwa hakika huu ni ulimwengu
maridhawa na hawakukosea walionena kwamba dunia hadaa ulimwengu shujaa.
Stori
ya kusikitisha, inatokea nchini Marekani ambako kijana Justin Street,
amepoteza maisha akiwa kwenye jaribio la kuongeza ukubwa wa nyeti yake.
Habari
kamili ipo hivi; Justin, 22, akiwa baba wa watoto wawili alikwenda kwa
mwanamama Kasia Rivera ,35, aliyejitangaza kuwa ni mtaalamu wa tiba za
kuongeza ukubwa wa nyeti za kiume.
Kasia
aliweka matangazo barabarani kuwa anayo tiba ya kuongeza ukubwa wa
nyeti za kiume, hivyo kumfanya Justin ahamasike kwenda kupata dawa hiyo
ili kujiongezea ushababi.
Wanasema
tamaa mbele mauti nyuma, ndivyo ilivyotokea kwa Justin, kwani baada ya
kuomba dawa ya kuongeza ukubwa wa maumbile yake ya kiume, alidungwa
sindano yenye madini ya silikoni.
Madini
hayo, alidungwa kwenye nyeti yenyewe na baada ya muda mfupi, hali ya
afya yake ilibadilika kuwa mbaya, alizorota na siku iliyofuata alifariki
dunia.
Kutokana
na tatizo hilo, Kasia alifikishwa mahakamani kwa kesi ya mauaji
akituhumiwa kufungua zahanati bubu ndani ya nyumba yake iliyopo New
Jersey, vilevile kutoa tiba za kiafya wakati hana taaluma hiyo wala
leseni ya kuendesha kazi hiyo ya utoaji huduma za afya.
Kasia
alipandishwa kizimbani wiki iliyopita, uchunguzi wa maiti umethibitisha
kwamba Justin alifikwa na mauti baada ya madini ya silikoni aliyodungwa
kwa sindano kuziba njia za mishipa ya damu.
Mmoja
wa madaktari waliomfanyia uchunguzi Justin alisema kuwa hii ni mara ya
kwanza kusikia silikoni inayotumika kuongeza ukubwa wa matiti ya
wanawake imetumika kwenye kuongeza ukubwa wa uume.Kasia, amekana
kuhusika na mauaji.
Social Plugin