Jeshi la polisi mkoa wa Mara limewakamata watu saba wakiwemo viongozi wawili wa Serikali ya kijiji cha Park Nyigoti katika kata ya Ikoma wilayani Serengeti mkoani Mara baada ya kutuhumiwa kuwakamata na kuwafunga vitambaa usoni watu wanane wanaowatuhumu kwa uchawi kisha kuwachapa viboko na kusababisha vifo vya watu watano.
Kaimu kamanda wa polisi mkoa wa Mara,kamishina msaidizi wa jeshi
la polisi ACP Ernest Kimola,amesema katika tukio hilo
limesababisha watu wengine watatu kujeruhiwa na viboko hivyo na
kulazwa katika hospitali teule ya Nyerere DDH Mjini Mugumu wilayani
Serengeti.
Amesema mbali na mwenyekiti na mtendaji wa serikali ya kijiji
kukamatwa pia viongozi wawili wa jadi wamekamatwa wakihusishwa na mauaji
hayo.
Amesema kabla ya kuwakamata wananchi hao wakiwa katika miji yao
kisha kuwafunga vitambaa usoni na kuwachapa viboko hadi kufa kwa
madai ya kujihusisha na vitendo vya ushirikina,viongozi hao jadi kwa
kushirikiana na Serikali ya kijiji waliitisha mkutano kwa lengo la
kuwabaini watu wanajihusisha na ushirikiana ambao umesababisha mvua
kutonyesha kijijini hapo ambapo watu wanane walitajwa katika
mkutano huo.
Kaimu kamanda huyo wa polisi mkoa wa Mara,amewataja waliouawa
katika tukio hilo lililotokea alfajiri ya tarehe 2.3.2015 kisha miili yao
kutupwa karibu na miji yao kuwa ni Nyahita Nyambeho,Nyasari
Holela,Joseph Msoba,Nyangi Nyakitambara na Nyangi Kanyaro wote wakazi
wa kijiji hicho ambapo Raphael Holela,Masenze Nyamsero na Elizabeth
Mwita wamelazwa katika hospitali ya Nyerere DDH baada ya kuchapwa
viboko na kujeruhiwa vibaya.
Hadi sasa jeshi la polisi kutoka makao makuu ya mkoa wa Mara
kwa kushirikaina na polisi mjini wilayani Serengeti wanaendesha na
operesheni kali katika kuwasaka watu wote walihusika kufanya mauaji hayo
ya kinyama.
via>>ITV
Social Plugin