Wachezaji watano wa kilabu ya Kano
Pillars nchini Nigeria walipigwa risasi na wapiganaji katika shambulizi
lillolenga msafara wa kilabu hiyo wakati wachezaji hao walipokuwa wakielekea
Owerri katika mechi ya ufunguzi wa Ligi kuu nchini Nigeria.
''Wachezaji watano walijeruhiwa
kutokana na shambulizi la risasi .
Wachezaji hao ni Gambo,Ogbonaya,Eneji Otekpa
na Murtala Adamu'', ulisema ujumbe wa mtandao wa twitter wa kilabu hiyo.
Wapiganaji hao pia walichukua simu
pamoja na vitu vyengine muhimu vya wachezaji hao.
Mechi iliokuwa ichezwe siku ya
jumamosi kati ya timu hiyo na ile ya Heartland imeahirishwa mara moja.
Kilabu hiyo ya Kano Piilars ilikuwa
ndani ya basi lililowabeba wachezaji 25,ikiwemo wachezaji 18,wakati wa tukio
hilo lililotokea mwendo wa saa saba na robo saa za Nigeria.
Wachezaji waliojeruhiwa kwa sasa
wanaendelea kupokea matibabu katika kituo cha matibabu cha Lokoja.
Siku ya ijumaa beki wa kilabu hiyo
Reuben Ogbonnaya aliiambia BBC kwamba anamshukuru Mungu kwa kumuezesha kuishi
kwa sababu hajui ni nini kingetokea.