Huenda utofauti wa tamaduni na mazoea ya
watu inafanya baadhi ya vitu pia kutofautiana.. zipo story za watu kula
mbwa na wanyama wengine, huku kwetu sio kawaida.
Kumbe China kuna soko la nyama ya punda?
Kuna maeneo ukienda utakuta punda wanatumiwa kubebea mizigo basi,
lakini kwa China punda ni nyama yenye soko kubwa tu.
Eneo la Maraigishu mji wa Naivasha, Kenya
kuna story ya ujenzi wa eneo la kiwanda cha machinjio ya punda kuelekea
kukamilika, ambapo tayari nyama hiyo ina soko la uhakika ndani ya
China.
Msimazi wa ujenzi huo Stephen Kairuki
amesema ujenzi huo umekamilika kwa 80%, eneo hilo litakuwa na Ofisi za
kiwanda hicho pamoja na maabara maalum ya kupima nyama kabla ya
kupakiwa, pia kutakuwa na mashine maalum ya kuchinjia punda na kuwachuna
ngozi.
Fundi huyo amesema wanakijiji wa eneo hilo watapewa punda wawili wa kufuga; “sio
kila mtu bali wakulima wa eneo hili watapewa punda wa kike na wakiume,
wakulima wanatarajiwa kuwafuga na kuwauzia kiwanda hicho kila
wanapokomaa“
Kutokana na mahitaji ya soko la nyama
hiyo China, kwa siku watatakiwa kuchinjwa punda 70, mbali na uhitaji wa
nyama pia kuna wafanyabiashara waliotoka Marekani ili kuingia
makubaliano ya kununua ngozi ya mnyama huyo kwa ajili ya kutengenezea
dawa ya vipodozi vya wanawake.
Kingine kitakachowanufaisha wanakijiji
kutoka kwenye kiwanda hicho ni huduma ambazo watasogezewa kutokana na
mradi huo kuwa kwenye kijiji hicho ikiwemo huduma ya maji, hospitali na
ajira kwa zaidi ya vijana 100.
Ufunguzi wa mradi huo utafunguliwa ndani ya kipindi cha miezi miwili kuanzia sasa.
Hizi ni baadhi ya picha kutoka Kenya kwenye mradi huo.