NB-Picha haihusiani na habari hapa chini |
Wakazi
wa Kijiji cha Ivaini Kenya wamejawa na hofu baada ya nyumba ya mzee
mmoja kuteketezwa kwa moto na viumbe visivyoonekana ambapo ishu hiyo
inahusishwa na imani za kishirikina.
Mzee huyo Mukai Kimanzi
amesema nyumba yake iliteketezwa na majini yanayoiandama familia yake
na yamekuwa yakimkosesha usingizi, yanamtia hofu kwa kuwapiga makofi
wakiwa usingizini.
“Waliniambia
waliona moto tu unachoma kila kitu kwa kweli nyumba.. moja imechomeka
na nyingine bado zinachomeka, kulingana vile mimi naona, mimi naona ni
mapepo tu” Mzee Mukai Kimanzi.
Majirani wa eneo hilo wamesema nyumba
hiyo imeteketezwa na mapepo mabaya na kudai kuwa huwa hali inakuwa
tofauti inapotimia saa moja usiku, yeyote atakaesogea eneo hilo
anarushiwa mawe na majini hayo.
Mzee huyo amelazimika kuondoka nyumbani
kwake na kuishi kwa ndugu yake ambae nae anataka kumfukuza mzee huyo
kutokana na hofu kwamba atavamiwa na majini hayo.
Social Plugin