Wadau wa Forbes
wamekuja na ripoti yao nyingine ya utaftii ndani ya 2015, kama
haujafahamu ni kwamba idadi ya matajiri wenye asili ya Afrika ni 11 kati
ya mabilionea wote 1,826 duniani.
Jina la Aliko Dangote
sio geni kulisikia, ni tajiri ambaye yuko kwenye namba moja AFRIKA,
anatokea Nigeria, ni mfanyabiashara na muwekezaji mkubwa katika miradi
kama ya Cement, Sukari na miradi mingine, huyu unaambiwa ndio tajiri
namba moja mwenye asili ya Afrika duniani.
List ya mabilionea wote kumi hii hapa;
No.1: Aliko Dangote, raia wa Nigeria ambaye ni mfanyabiashara wa mafuta, cement ambapo moja ya miradi yake mikubwa unajengwa Tanzania.
No.2: Mohammed Al-Amoudi. Huyu ni raia wa Ethiopia, mfanyabiashara mkubwa wa mafuta.
No.3: Mike Adenuga,
raia wa Nigeria ambaye biashara yake kubwa ni mafuta na huduma za
Mawasiliano, anamiliki mtandao wa simu wa Globacom, huu ni wa pili kwa
ukubwa Nigeria.
No.4: Isabel Dos Santos, raia wa Angola ambaye ni mtoto wa Rais wa zamani wa nchi hiyo, Jose Eduardo dos Santos. Naye ni mwekezaji wa miradi mbalimbali ikiwemo Kampuni za Mawasiliano na Mabenki pia.
No.5: Oprah Winfrey, ni Mmarekani ambaye sehemu kubwa ya kipato chake inatokana na TV show yake ambayo ni moja ya shows maarufu duniani.
No.6: Patrice Motsepe, raia wa South Africa. Ni mmoja wa wawekezaji wakubwa Afrika Kusini kwenye biashara ya madini.
No.7: Folorunsho Alakija.
Raia wa Nigeria ambaye aliacha kazi ya usekretari na kujifunza masomo
ya masuala ya fashion Uingereza, kwa sasa ni fashion na kuwekeza kwenye
miradi ya mafuta kumemfanya kuingia kwenye list hii.
No.8: Theophilus Danjuma.
Huyu ni mtu wa nne kwenye list hii kutoka Nigeria, aliwahi kuwa Waziri
wa Ulinzi Nigeria, kwa sasa utajiri wake unatokana na biashara zake
kuwekeza kwenye mafuta, pamoja na makampuni ya usafirishaji wa majini.
No.9: Mo Ibrahim. Anaishi Uingereza, ni mmoja ya wawekezaji kwenye makampuni ya mawasiliano pia, alikuwa mmiliki wa Kampuni ya Celtel.
No.10: Tony Elumelu. Raia wa Nigeria, mtaalamu wa masuala ya uchumi na mfanyabiashara.
Social Plugin