Ugumu wa maisha unaongeza ubunifu,
ubunifu mwingine unakuweka pabaya.. huu wa huyu jamaa sidhani kama
tunaweza kuuita ni ubunifu ila jamaa aliamua tu atumie njia hii ili
apate tu njia ya kupata mkate wa siku.
Mmiliki wa Bar ya Siaya, Kenya
alimshtukia jinsia ya mmoja ya wahudumu wake wa Bar kwamba jinsia yake
sio ya kike.. Akatoa taarifa Polisi kuhusu mhudumu huyo, walipokuja
kumpekua jamaa alijitetea kwamba ana jinsia mbili.
Jamaa huyo anaitwa Michael Obiero alikamatwa baada ya kufanya kazi kwa siku mbili kwenye Bar hiyo akijitambulisha kwa jina la Brenda na pia alikuwa akilala chumba kimoja na wahudumu wengine wa kike.
Polisi walimlazimisha avue nguo zake ili
wamkague, wakaona hakuwa na muonekano wa jinsia ya kike, wanaendelea na
upelelezi ili kujua ukweli japo Mkuu wa Polisi Kaunti ya Bondo amesema
hata mmiliki wa Bar hiyo huenda akawa na makosa ya kumuajiri jamaa huyo
bila kumkagua.
Social Plugin