Majaji watatu wamefutwa kazi kwa kutumia muda wao afisini kutizama filamu za ngono.
Jaji Timothy Bowles anayesikiza kesi za wilaya , jaji wa maswala ya uhamiaji Warren Grant na jaji Peter Bullock wamefutwa kazi.
Majaji hao walipatikana na hatia ya kutumia mtandao rasmi wa mahakama kwa mujibu wa wachunguzi wa idara ya mahakama.
Maafisa
hao wanasemekana kuwa walitazama mitandao yenye filamu za ngono huku
wakifahamu vyema kuwa ilikuwa ni ukiukaji wa sheria za matumizi kwa
mujibu wa msimamizi wa idara hiyo ya Mahakama.
Hata hivyo kiongozi
wa idara ya mahakama hiyo ya Uingereza na jaji mkuu waliwapata na hatia
ya kwenda kinyume cha maadili ya mahakama.
Jaji wa nne Andrew Maw aliamua kustaafu mwenyewe wakati uchunguzi huo ukiendelea badala ya kufikishwa kizimbani.
Mwandishi
wa BBC wa maswala ya kisheria Clive Coleman kuwa makosa hayo yalikuwa
makubwa sana katika mizani ya uadilifu wa majaji.
Aidha hakuna hata mmoja wao atakayeruhusiwa kufanya kazi katika idara ya mahakama tena.
Via>>>BBC
Social Plugin