Matumizi ya condom imekuwa ikishauriwa
sana kwa muda mrefu kama njia ya kusaidia mtu kujikinga na maradhi ya
kuambukiza kati ya watu walio kwenye uhusiano.
Kutoka Kiyindi, Kampala Uganda stori
ambayo iko tofauti kidogo ni hii ishu ya watu kubuni kitu tofauti,
badala ya condom wao wanatumia condom bandia, wamezibuni wenyewe
kutokana na mifuko ya plastiki wanaziita ‘buveera’.
Mahitaji ya condom ni makubwa lakini
wenyeji wa eneo hilo wamesema hali ngumu ya kimaisha imefanya washindwe
kumudu gharama za kununua kinga hizo.
Ripoti ya Tume ya kuthibiti Ukimwi ya
mwaka 2013 ilionesha Uganda inahitaji condom milioni 20 kila mwezi, hata
hivyo zinazopatikana hazitoshi, kingine ni kwamba condom zinauzwa bei
ambayo kwa watu wenye kipato kidogo hawawezi kumudu.
Mfanyakazi
mmoja wa kituo cha Afya cha jamii amesema kiwango cha maambukizi UKIMWI
na kuenea magonjwa mengine ya zinaa katika Wilaya hiyo yako juu sana
ambapo ishu ya wahisani kupunguza usambazaji baada ya mtafaruku
uliotokana na Serikali kuzuia uhusiano wa jinsia moja.
Social Plugin