HILI NDIYO SHIMO LILILOSABABISHA AJALI HUKO IRINGA, VIFO VYAONGEZEKA SASA NI 50
Thursday, March 12, 2015
Shimo
hili katikati ya barabara ndilo linasadikika kuwa chanzo cha ajali
iliyoua watu 43 na zaidi ya 20 kujeruhiwa, katika eneo la Changarawe
Mafinga Iringa.
Idadi ya Vifo katika ajali iliyotokea jana mjini Mafinga Mkoani
Iringa imeongezeka na kufikia watu 50 baada ya mtu mmoja kufariki dunia
usiku wa kuamkia leo na miili mingine saba ambayo jana haikuhesabiwa,
kugundulika mchana wa leo.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Iringa
Kamishna msaidizi wa Polisi Ramadahani Mungi amesema kuwa miili hiyo
saba iliingizwa katika majokofu moja kwa moja kutoka katika eneo la ajali, hali iliyosababisha isihesabiwe huku akitaja majeruhi kuwa ni 22 na wawili kati yao wakiwa katika hali mbaya.
Katika hatua nyingine Mwenyekiti wa chama cha NCCR Mageuzi James Mbatia
ameitaka serikali kuchukua hatua kwa kila aliyehusika na kutokea kwa
ajali hiyo, huku akitaka ufanyike uchunguzi wa kina ikiwa ni pamoja na
kuchukua hatua za kutoruhusu malori kusafirisha mizigo katika barabara
moja na mabasi ya abiria
Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Social Plugin