HOT News!! ASKARI POLISI WAWILI WAUAWA KWA KUPIGWA RISASI TANZANIA

 
Askari polisi wawili waliokuwa katika kizuizi cha barabara katika kijiji cha
Kipara mpakani mwa  wilaya ya Mkuranga mkoani Pwani wameuawa kwa kupigwa
risasi huku askari mmoja akijeruhiwa baada ya kupigwa risasi kwenye paja  na
Watu wanaosadikika kuwa ni majambazi na kisha kupora bunduki moja.

Tukio hilo limetokea siku ya Jumatatu ,tarehe 30 Machi 2015 majira ya saa moja usiku
katika kizuizi kilichopo katika kijiji cha Kipara wilaya ya Mkuranga mkoani
Pwani sehemu inayotenganisha mkoa wa Pwani na Dar es salaam ambapo watu
wasiojulikana wakidaiwa kuwa na panga walivamia ghafla askari hao waliokuwa
katika lindo na kuwauwa askari wawili kwa kuwapiga risasi huku askari mmoja
akijeruhiwa kwa kupigwa risasi katika sehemu ya paja.

 
Licha ya ITV kufika katika kituo kikuu cha polisi kati jijini Dar es salaam
ili kuzungumza na kamishna wa polisi kanda maalum ya Dar es salaam Suleiman
Kova kuhusu tukio hilo la askari wa kanda yake,kamishana kova alikataa
kuzungumza huku akisema anayetakiwa kuzungumza ni kamanda wa polisi mkoa wa
Pwani Urlich Matei .

Hata hivyo  licha ya kudaiwa kuwepo  jijini Dar es salaam
na kupigiwa simu na mwandishi wa ITV lakini alipomaliza kutaja jina lake tu
alikata simu na kisha kutuma ujumbe wa sms kwamba atafutwe kamanda wa polisi
mkoa wa Temeke ambapo licha ya ITV kufika Temeke na kukuta kamanda wa mkoa huo
hayupo na kuomba kuzungumza na kamishna Simon Siro lakini naye akakataa
kuzunguimzia tuki hilo.

ITV ilifika katika hospitali ya Temeke alipolazwa askari aliyejeruhiwa kwa
Kupigwa risasi kwenye paja na kuzungumza na mganga mfawidhi wa hospitali hiyo
Dk.Amani Malima ambaye alikiri kumpokea askari huyo huku askari huyo
Sajent Ally Jumamne kutoka kituo cha Mbagala akisema anaendelea vyema kwa
sasa.

Miili ya askari wawili waliojulikana kwa majina ya Sajent Francis na Coplo
Michael waliopoteza maisha katika tukio hilo inadaiwa kuhifadhiwa katika
Hospitali ya taifa ya Muhimbili jijini Dar es salaam.

Hata hivyo baadaye kamishna wa polisi kanda maalum ya Dar es salaam Suleiman
Kova alizungumza na waandishi wa habari na kusema kuwa jeshi la polisi linaendesha oparesheni maalum kuwasaka na kuwakamata wahusika wa tukio hilo.

Via>>ITV

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post