Rais
Jakaya Kikwete amesema amesikitishwa na kushangazwa kwa kitendo cha
baadhi ya viongozi wa dini kutoa matamko kwa waumini wao ya kuwataka
kupiga kura ya hapana kwa katiba inayopendekezwa na kuongeza kuwa
hakuwahi kudhani wala kufikiri kuwa kwa viongozi aliowaheshimu kama
wangeweza Kufanya jambo kama hilo kwa waumini wao.
Mh.Kikwete ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na viongozi wa dini
kupitia kamati ya amani ya mkoa wa Dar es Salaam ambapo amesema kitendo
walichofanya viongozi hao wa dini kingeweza kuwa na tija kama katiba
inayopendekezwa ingekuwa inawanyima uhuru wa kuabudu.
Na kuhusu mahakama ya kadhi Mh.Kikwete amesema serikali haitaanzisha ila waislamu wenyewe wana uhuru wa kuwa nayo amala.
Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mh.Said Meck Sadick
amesema uwepo wa hali ya utulivu hasa katika mkoa wa Dar es Saam
imewezekana kutokana na viongozi wa Dini kuwa naumoja ambao kila
mara wamekuwa mstari wa mbele kusaidia amani idumu nchini.
Kwa upande wake mwenyekiti wa kamati hiyo Sheikh mkuu wa mkoa wa
Dar es Salaam Alihadi Mussa Salum amesema mkutano huo unalengo la
kujadili mambo makubwa yanayolihusu taifa ambapo makamu Mwenyekiti
wa kamati hiyo askofu Valentino Mokiwa amesema bado ipo
changamoto ya matumizi ya Demokrasia iliyopo nchini.
Social Plugin