Baada ya kutemwa na CHADEMA, Zitto Kabwe ameenda jimboni kwake Kigoma Kaskazini kuzungumza na wananchi wake.
Pichani ndiyo mapokezi aliyopata huko jimboni, watu wengi wamejitokeza
kumpokea na kelele zikisikika ..ZITOO...ZITOOO..ZITOOO...
Zitto Kabwe hivi punde katika ukurasa wake wa Twitter na Facebook ameandika maneno yafuatayo
"Leo
nimekutana na wazee wa jimbo la kigoma kaskazini na wawakilishi wa
vijiji vyote 45, nimewaaga rasmi kuwa sitagombea ubunge jimbo hilo"
Ujumbe mwingine alioandika huu hapa
"Nimewashukuru kwa kunipa fursa kutoa utumishi wangu kwao kwa miaka 10. Kwa niaba yao wote Mzee Mahmoud Bikulako alifanya dua na maombi rasmi"
Mwingine huu hapa
"Wazee wamenibariki kuchukua maamuzi yanayofaa kulingana na hali ya kisiasa inayoendelea hivi sasa"
"Kisheria, kikatiba, kikanuni Mimi bado ni mwanachama wa chama nilichotumia kuingia bungeni mwaka 2010"
Social Plugin