Hot News!! ZITTO KABWE ATANGAZA KUTOGOMBEA TENA UBUNGE

Baada ya kutemwa na CHADEMA, Zitto Kabwe ameenda jimboni kwake Kigoma Kaskazini kuzungumza na wananchi wake. 




Pichani ndiyo mapokezi aliyopata huko jimboni, watu wengi wamejitokeza kumpokea na kelele zikisikika ..ZITOO...ZITOOO..ZITOOO...
Zitto Kabwe hivi punde katika ukurasa wake wa Twitter na Facebook ameandika maneno yafuatayo
"Leo nimekutana na wazee wa jimbo la kigoma kaskazini na wawakilishi wa vijiji vyote 45, nimewaaga rasmi kuwa sitagombea ubunge jimbo hilo"



Ujumbe mwingine alioandika huu hapa
"Nimewashukuru kwa kunipa fursa kutoa utumishi wangu kwao kwa miaka 10. Kwa niaba yao wote Mzee Mahmoud Bikulako alifanya dua na maombi rasmi"

Mwingine huu hapa
 "Wazee wamenibariki kuchukua maamuzi yanayofaa kulingana na hali ya kisiasa inayoendelea hivi sasa" 


"Kisheria, kikatiba, kikanuni Mimi bado ni mwanachama wa chama nilichotumia kuingia bungeni mwaka 2010"

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
أحدث أقدم