Baraza la Kilimo Tanzania (ACT) limekitaka chama cha siasa cha ACT –
Tanzania kutotumia jina hilo kwa kuwa tayari baraza hilo limekwsha
sajili jina la ACT kama kifupi cha jina la Baraza hilo.
Akizungumza leo katika kipindi cha Hotmix cha EATV kinachoruka kila
Jumatatu hadi Ijumaa saa 12:00 hadi saa 2:00 jioni, Mwenyekiti wa Baraza
hilo Dkt Sinare Yusuf Sinare amesema kuwa jina ACT linatambulika kama
kifupi cha Agricultural Council of
Tanzania na kwa mujibu wa taratibu za hati miliki, jina hilo (ACT)
halitakiwi kutumika na watu wengine hata kama litaambatanishwa na maneno
mengine.
“Hata kama
wakiongeza maneno, bado kuna ACT, hiyo ni nembo yetu, tumekwisha andika
barua kwenda kwa msajili wa vyama vya siasa, pia tumeandika barua kwenda
katika chama hicho lakini bado hatujapata majibu, nimekwisha ongea na
Zitto Kabwe kuhusu hilo na kumweleza kuwa wanatakiwa kurekebisha kabla
hatujaenda hatua za juu zaidi(Mahakamani) ambazo ni ghali.” Amesema Dkt
Sinare.
Social Plugin