Wanajeshi wa Iraq na wapiganaji
wanaopigana na wanamgambo wa Islamic State karibu na mji wa Tikrti
wanasema kuwa kaburi na la rais wa zamani wa nchi hiyo Saddam Hussein
karibu limeharibiwa kabisa.
Picha za shirika la habari za AP
zilionyesha mabaki ya kaburi hilo lililojengwa kwa njia ya kifahari
lililo katika kijiji cha al-Awja.
Aidha zinaonesha picha za Saddam
zikiwa zimeondolewa na mahala pake kuwekwa picha za viongozi wa
wapiganaji ikiwemo picha ya jenerali wa Iran Qassem Soleimani
anayewashauru wapiganaji wanaopigana vita na islamic state.
Mwaka uliopita jamii ya wasunni wanaokaa katika eneo hilo liliondoa
mwili wa kiongozi huyo wa Iraq ambaye kungolewa kwake madarakani na
majeshi ya muungano yaliongozwa na Marekani iliitumbukiza taifa katika
vita ambavyo vimechacha hadi leo.
Haijulikani hadi wa leo ulizikwa wapi mwili huo.
Mwandishi
wa BBC nchini Iraq anasema kuwa kuna shauku kuwa huenda wapiganaji wa
Shia ndio walioharibu kaburi hilo ilikulipiza kisasi cha mateso
waliyopita mikononi mwa kundi la Islamic state na wapiganaji wa Sunni.