Mahakama ya wilaya ya
kahama mkoani Shinyanga Juzi imemuhukumu kwenda jela miaka 20 Ally
Sanyiwa (24) kwa kosa la kumuoa dada yake Mektilda Sanyiwa(20) mkazi wa
Chela.
Imedaiwa mahakamani hapo
na mwendesha mashitaka wa polisi Koplo Evodia mbele ya hakimu mfawidhi
George Mariki kuwa mtuhumiwa huyo alitenda kosa hilo mwezi machi mwaka
huu.
Aidha koplo Evodia
ameiambia mahakama hiyo kuwa mtuhumiwa huyo aliweza kumtorosha dada yake
na kisha kumpeleka katika kijiji cha Mazimba na kuishi naye.
Wazazi wa Mektida ambaye
ni mlemavu wa ngozi (albino) wamesema kuwa mara baada ya binti yao
kutoweka nyumbani walipata hofu na kuanza kumtafuta mpaka alipopatikana
akiwa anaishi nyumba moja na kijana wao.
Mahakama hiyo imetoa
hukumu kwa mtuhumiwa huyo mara baada ya kukiri kutenda kosa hilo ambalo
ni kinyume na maadili ya kitanzania.
via>>Farajimfinanga.com
via>>Farajimfinanga.com
Social Plugin