Matukio ya mauaji ya watu wenye ulemavu ya ngozi yanaendelea kujitokeza nchini, ni wiki moja baada ya mtoto mmoja Yonana Bahati kuuawa Geita na watu wasiofahamika na leo kuna mlemavu mwingine ameripotiwa kukatwa mkono huko Sumbawanga.
Leo
kwenye Power Breakfast Clouds FM, kulikuwa na mazungumzo na
Mkurugenzi wa shirika linalotetea haki za watu wenye ulemavu wa
ngozi la Under The Same Sun, Vicky
Mketema, amezungumzia jinsi ukatili huo unavyofanyika;
“Watu ambao wanataka madini
ule mguu wanasema kwamba unakuwa kama ni chombo cha kuangalia madini yako wapi
katika mwamba.. wanachokifanya ni kwamba huu mguu unapelekwa katika eneo
na kuna kelele ambazo zinatokea wanazozisema wao kama vile kelele za kwenye
redio wakati unatafuta stesheni, kwa hiyo iyo kelele inapotokea ndipo ambapo
mganga anawaambia kwamba anze kuchimba“
Anaweza kuambiwa achukue damu ambayo awe amekuja nayo au ni mganga
kampatia lakini pia ni damu ya binadamu, lazima kafara ya binadamu itolewe ile
damu sasa mganga anasema kwamba anaimwaga katika eneo moja halafu ule
mchuruziko wa damu ndio unaofuatwa pale ambapo hiyo damu itatuama katika huo
mchuruziko basi ndipo hapo huyu mtu wa madini ataambiwa kwamba anza kuchimba
katika eneo hili“
Vicky Ntetema
“..wakati mwingine
wanasema kwamba wanapoishiwa viungo wanawaomba wenzao.. kuna muungano wa
waganga wa kienyeji ambao wanatumia viungo vya watu wenye Albinism
anapoishiwa hapa anamuomba mwenzake Kijiji cha pili au kama sio Kijiji cha pili
anakwenda hata nchi jirani, hayo yote ni maneno yanayosemwa na waganga wenyewe
” maelezo ya Vicky Mketema.
Mtetema amesema nywele za albino pia huwa zinakaangwa na kutumiwa na wavuvi kuvuta samaki kwenye maji.
Mtetema amesema nywele za albino pia huwa zinakaangwa na kutumiwa na wavuvi kuvuta samaki kwenye maji.
Nimekuwekea hapa mazungumzo yote,
unaweza bonyeza play kusikiliza.
Social Plugin