Wakati jeshi la polisi katika mikoa ya kanda ya
ziwa likiwa katika msako mkali wa kuwakamata waganga wa kienyeji wanaopiga
ramli chonganishi katika hali isiyokuwa
ya kawaida Chama cha Mapinduzi wilayani Itilima Mkoani Simiyu kimemtaka Mkuu wa polisi Mkoani hapa
kusitisha msako huo.
Mbali na kumtaka kusitisha mara moja zoezi la
msako huo chama hicho kimemtaka kutoa muda wa kutosha kwa waganga wa jadi, ili
kupatiwa leseni kwa ajili ya kutambulika kazi zao na serikali ili wasikamatwe
katika msako huo.
Agizo hilo limetolewa jana na Mwenyekiti wa CCM
Wilayani humo Mohamudu Mabula, wakati wa mkutano wa waganga wa jadi uliofanyikia katika viwanja vya shule ya sekondari Lagangabilili.
Mabula alimtaka Mkuu huyo wa Polisi Mkoa Charles
Mkumbo ambaye alihudhulia Mkutano huo, kusitisha zoezi hilo ikiwa pamoja na
kutoa muda kwa waganga hao kwa kile alichoeleza baadhi yao wamekamatwa
kutokana na kukosa leseni lakini hawajihusishi na upigaji wa ramli.
Alieleza kuwa anatambua umuhimu wa agizo la
kiongozi wake Rais Jakaya Kikwete, lakini juu ya uendeshaji wa zoezi hilo
amelipinga kutokana na waganga wengi kutopewa muda wa kujiandikisha ili
kupatiwa leseni hizo.
"zoezi hili linataka kutukumbusha oparesheini
kimbunga kwa wahamiaji haramu pamoja na kukamata majangili..operesheni hizi
zimeondoka na viongozi wengi wachapakazi..sasa hatutaki chama kurudia
makosa..tunataka operesheini zifanyike kwa amani na siyo kuwashtukiza watu”
Alisema Mabula.
Alieleza kuwa maagizo ambayo yamekuwa yakitolewa
na viongozi wao ngazi za juu kwa upande wa serikali, yamekuwa yakiwapatia
wakati mgumu viongozi wa chama ngazi za mkoa na wilaya kutokana na maagizo hayo
kutekelezwa kwa nguvu.
“ sisi kama chama tumeanza kupata malalamiko
kutoka kwa wapiga kura wetu..wanasema CCM inataka kuwafukuza waganga wa
jadi…kwa hili hatukubali tulalamikiwe tunachoitaji msako ufanyike lakini kwa
amani na watafutwe wapiga ramli tu na siyo waganga wote” Alisema
Kiongozi huyo akishangiliwa na umati wa waganga wa
jadi zaidi ya 200 waliohudhuria mkutano huo na alisema kuwa yuko tayari kwenda
jela kwa niaba ya waganga katika wilaya hiyo, ikiwa zoezi hilo halitasitishwa
ikiwa pamoja na waganga wake kutopewa muda wa kutosha kwa ajili ya kupatiwa
leseni hizo.
Mbali na kauli hizo mwenyekiti huyo alisema kuwa
atapambana hadi ngzi za juu kuhakikisha waganga ambao wanafanya kazi yao kwa
kufuata misingi ya sheria na kanuni za nchi hawaonewi kwa kisingizio cha kupiga
ramli chonganishi.
Rpc
atii amri, asitisha operaisheni.
Kutokana na kauli ya kiongozi huyo Mkuu huyo wa
polisi aliposimama kujibu hoja mbalimbali alitamka kusitishwa kwa zoezi hilo
katika wilaya hiyo, na kutoa muda wa mwezi mmoja kwa kila mganga kuhakikisha
anapatiwa leseni.
Mkuu huyo wa Polisi aliwataka waganga hao
kuhakikisha ndani ya muda huo wanakamilisha taratibu zote za kupatiwa leseni,
huku akieleza kuwa mara baada ya muda huo kumalizika operesheni itaanza upya.
“ tumesitisha zoezi kama alivyosema mwenyekiti na
tunatoa muda wa mwezi mmoja..lakini baada ya muda huo tutaanza
msako..ninachowaomba waganga nyote nendeni kwa viongozi wenu mkajiandikishe ili
taratibu za leseni ziweze kufanyika.
Alisema kuwa anafahamu taratibu wa kupatiwa leseni
hizo unachukua muda mrefu, ambapo aliwataka kufanya zoezi la kujiandikisha ili
muda aliotoa ukimalizika ambao watakakuwa wamejiandikisha na kutambulika kwa
viongozi wa serikai ngazi zote hawatakamatwa.
Shimautita
waunga mkono msako.
Hata hivyo shirika la maendeleo la utafiti tiba
asili Tanzania limeunga mkono serikali kuanzisha zoezi hilo la msako mkali la
kuwatafuta wapiga ramli chonganishi.
Katibu Mkuu wa shirika hili Dk Aron Machokosi alisema
kuwa kutokana na hali ilivyo hivi sasa kwa watu wenye ulemavu wa ngozi pamoja
na vikongwe operesheini hiyo imekuwa katika muda muhafaka.
“ tunaipongeza serikali kwa uamuzi wake huo..ni
lazima waganga wa jadi kufuata misingi ya sheria na kanuni za nchi…tunachowataka
waganga wote nchi nzima wajiandikishe katika sehemu husika kwa ajili ya
kujipatia leseni” Alisema Machokosi.
Hata hivyo katibu huyo alimshangaa mwenyekiti wa
CCM kuagiza kusitishwa kwa zoezi hilo, ikiwa pamoja na mkuu wa polisi kutii amri
hiyo na kutoa muda huo, kwa madai kuwa agizo hilo limetolewa na kiongozi wa
nchi hivyo linatakiwa kufanyiwa kazi bila ya mzaha.
Hata hivyo mikutano ya waganga wa jadi inafanyika
huku kukiwepo msako mkali kwa wapiga ramli chonganishi ambao wameelezwa kuchochoa
mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi (Albino) pamoja na vikongwe.
via>> http://simiyunews.blogspot.com
via>> http://simiyunews.blogspot.com
Social Plugin