KAMPUNI YA UUZAJI MAGARI NA MITAMBO GF TRUCKS & EQUIPMENT LTD YATOA MSAADA KWA WAHANGA WA MVUA MWAKATA KAHAMA
Monday, March 16, 2015
Hapa
ni ofisi za halmashauri ya manispaa ya Shinyanga ambapo leo Jumatatu Machi
16,2015,Kampuni ya uuzaji magari na mitambo nchini Tanzania GF Trucks &
Equipment Limited yenye makao yake makuu jijini Dar es salaam imekabidhi msaada
wa vitu mbalimbali kwa ajili ya wahanga wa mvua katika kijiji cha Mwakata
wilayani Kahama ikiwemo sabuni katoni 20,ndoo 20 za mafuta ya kula na sukari
kilo 140 vyote vikiwa na thamani ya shilingi milioni 1.2.
Pichani kushoto ni Mhandisi
mwandamizi idara ya Mauzo na Masoko kutoka kampuni hiyo Juma Hamsini akikabidhi ndoo ya mafuta ya kula kwa
kwa meya wa manispaa ya Shinyanga Gulamhafeez Abubakar
Mukadam ambaye ni mwakilishi wa wananchi atakayepeleka msaada huo kwa wahanga
wa mvua ya mawe na upepo iliyoua watu 46 hivi karibuni-Picha zote na Kadama Malunde-Shinyanga
Kulia ni diwani wa kata ya Kambarage kupitia CHADEMA Nyangaka Shilungushela akishuhudia tukio la makabidhiano hayo
Mhandisi
mwandamizi idara ya Mauzo na Masoko kutoka Kampuni ya uuzaji magari na mitambo nchini Tanzania GF Trucks &
Equipment Limited yenye makao yake makuu jijini Dar es salaam akikabidhi mfuko wa sukari wenye kilo 20 ikiwa ni miongoni mwa mifuko 7 ikiwa na jumla ya kilo 140 kwa ajili ya kusaidia wahanga wa mvua ya Tonado iliyonyesha katika kijiji cha Mwakata wilayani Kahama mkoani Shinyanga usiku wa kuamkia Machi 4,2015-Picha zote na Kadama Malunde-Shinyanga
Social Plugin