Kauli
hiyo ilitolewa jana na mwenyekiti wa CCM mkoa wa Shinyanga
Khamis Mgeja wakati akizungumza na wananchi wa kijiji cha Mishepo kata ya
Mwantini wilaya ya Shinyanga katika maadhimisho ya miaka 38 ya chama hicho.
Mgeja alisema kitendo cha viongozi wa CCM kuwachagulia wananchi wagombea wanaowataka wao ndiyo chanzo cha CCM kushindwa katika uchaguzi kwa baadhi ya maeneo katika uchaguzi wa serikali za mitaa uliopita.
Mgeja alisema katika
uchaguzi wa serikali za mitaa ilikuwa kama dakika 45 za kipindi cha kwanza na
sasa ni mapumziko kuelekea kipindi kingine cha dakika 45 ambacho ni kuelekea uchaguzi mkuu
mwaka huu 2015 hivyo kuwataka
WanaCCM kufanya tathmini ya kubaini kasoro na mafanikio ya uchaguzi wa serikali za mitaa uliopita.
WanaCCM kufanya tathmini ya kubaini kasoro na mafanikio ya uchaguzi wa serikali za mitaa uliopita.
“ Nawakumbusha wanachama na viongozi mtambue siasa ni sawa na
gemu la mchezo, sasa ni vyema benchi la ufundi ambalo ni halmashauri kuu za matawi,kata wilaya, mkoa
na mpaka taifa watumie kipindi hiki cha mapumziko kurekebisha kasoro
zilizojitokeza katika uchaguzi uliopita ili kujirekebisha katika uchaguzi mkuu
ujao na kupata ushindi wa kutosha’’,alieleza Mgeja.
Mwenyekiti huyo alisema silaha kubwa ya
ushindi ni kujenga umoja, mshikamo ndani ya chama na kuondoa sumu ambazo ni
mbaya na zinazopelekea kukigharimu chama kama zile za ubinafsi, chuki na makundi.
"Tuombe sasa wanachama wa CCM watimize wajibu wao kulinda
chama na kukitetea pia na kuyazungumza mafanikio yaliyopatikana katika kipindi cha miaka 38 ya CCM na kupata mafaniko makubwa ya kimaendeleo katika nyanja zote za elimu ,afya ,miundombinu ya barabara ,maji na nishati za umeme na huduma
mbalimbali za kijamii,"alieleza Mgeja.
Katika hatua nyingine alisema katika mafanikio hayo CCM mkoa
wa Shinyanga inawapongeza,madiwani wabunge ,Mheshimiwa rais Jakaya Mrisho Kikwete kwa
kutekeleza ilani ya CCM kwa mafanikio makubwa,na kuwafanya wanaCCM kutembea kifua
mbele .
Aidha Mgeja aliwataka viongozi na wana ccm kutotembea na
majina ya wagombea kwenye mikoba yao,na ni vema kama wapo wajitokeze wao wenyewe ili wananchi na wanachama wa CCM waweze kuwapima kwa
uwezo wao ,lakini watambue kuwa muda wa kampeni bado .
Na Kadama Malunde-Shinyanga
Na Kadama Malunde-Shinyanga