Kimenuka Geita!! WAGANGA WA KIENYEJI 32 WAKAMATWA WAKIHUSISHWA NA MAUAJI YA ALBINO NA VIKONGWE!!

Jeshi la polisi mkoa wa Geita limewakamata waganga wa kienyeji  32 wanaopiga ramli chonganishi katika msako uliofanywa hivi karibuni ili kuhakikisha mauaji ya vikongwe na watu wenye ulemavu wa ngozi yanakomeshwa kabisa.


Akizunguza na waandishi wa habari baada ya kufanya msako na kuwakamata waganga hao kamanda wa polisi mkoa wa Geita Sacp Joseph Konyo amesema waganga hao wamekamatwa wakiwa na vifaa mbalimbali ambavyo ni matunguri na ngozi  za wanyama kama vile simba chui na nyati vikiwa vimekaushwa.
 
 
 Kamanda  Konyo mesema sasa wakati umefika wa kuhakikisha mauaji yanayotokana na imani potofu za kishirikina yanakomeshwa na ili kuyakomesha watu wa kwanza kudhibitiwa ni waganga wa kienyeji wanaofanya shughuli zao pasipo kuzingatia sheria na taratibu zilizowekwa na nchi.
 
Kamanda Konyo amesema upo ushahidi wa wazi unaonyesha mahusiano ya karibu ya mauaji haya ya vikongwe na watu wenye ulemavu wa ngozi na waganga wa kienyeji kwani ndio wahusika wanaoagiza viungo vya Albino na ndio hao wanaopiga ramli za uongo kuonyesha kuwa vikongwe hasa wanawake ndio wachawi.
 
Ameongeza kuwa jeshi la Polisi haliwezi  kuhangaika na watu wengine wakati huku waganga ndiyo wanaosababisha mauaji hayo ya walemavu wa ngozi  na vikongwe  huku wakisababisha wananchi kuacha kufanya shughuli zao za kila siku
 
Kamanda Konyo amesema serikali haiwezi kuvumilia waganga wa namna hii wanaoipotosha jamii hivyo msako huu utaendeshwa katika mikoa yote Tanzania bara ili kubaki na jamii salama isiyokuwa na vitisho vya mauaji ya kikatili kama haya.
 
Baadhi ya wananchi mkoa wa Geita wameipongeza hatua ya serikali kuanza sasa kuwachukulia hatua watuhumiwa wote wanaopatikana na tuhuma za mauaji yanayotokana na mila potofu na ushirikina.
Na  Valence Robert -Malunde1 blog Geita

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
أحدث أقدم