Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

KIMINI CHA TRAFIKI HUYU CHAZUA GUMZO,WAHUNI WAMFANYIA MAMBO YA AJABU

Muonekano wa kimini alichokuwa amevaa trafiki.
Kimini alichovaa trafiki wa kike ambaye jina lake halikupatikana mara moja, kinadaiwa kuzua balaa huku wahuni wakimpigia miluzi.

 Tukio hilo lililojaza kadamnasi na kushuhudiwa na ‘shushushu’ wetu lilijiri wiki iliyopita maeneo ya Mwenge jijini Dar, majira ya asubuhi.

Bila kujua ‘amefotolewa’ trafiki huyo alikuwa amesimama pembeni akimtazama mwenzake wa kiume aliyekuwa akiongoza magari huku kimini chake cha sare ya kazi kikiwa kimepanda juu na kuonesha sehemu ya upaja wake wa haja.

“Jamani mbona majanga? Waone wahuni wanavyokitolea macho kimini cha trafiki na hapo amesimama. Akiinama kidogo tu mambo yote hadharani,” alisema mama aliyekuwa akiwashangaa raia walioacha kazi zao na kujadili kivazi hicho cha trafiki huyo.

“Tunachojua ni kwamba hizi sare huwa wanashonewa na serikali siyo kwamba wanashona wenyewe. Kazi yao inahitaji kufuata maadili kwa kuwa ni watumishi wa umma.

 “Itakuwa ameongezeka mwili kwa sababu mbali na kuwa kifupi pia kinambana kama kile cha trafiki mrembo wa nchini Kenya aliyeibua gumzo mwaka jana.

“Au inawezekana washonaji hawakumpima vizuri kwa sababu sketi zao zinatakiwa zifike chini ya magoti,” alisema jamaa mmoja aliyekuwa akijaribu kutafuta majibu ya kimini hicho.

Ili kupata mzani wa habari hiyo kuhusu mavazi ya trafiki wa kike hasa urefu wa sketi za trafiki wa kike, tulimtafuta Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Mohammed Mpinga lakini alipopigiwa simu, iliita mara kadhaa pasipo kupokelewa.
Via>>GPL

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com