Mwezi December 2014 kulikuwa na story ya mtuhumiwa mmoja kuuawa kwa kupigwa risasi wakati alipokuwa akijaribu kutoroka Mahakama ya Kisutu
kwa kuruka ukuta wa Mahakama hiyo, story kutoka Kenya leo inafanana na
hii.. inahusu mtuhumiwa mmoja kufanya jaribio la kutoroka kutoka Mahakama ya Machakos.
Mtuhumiwa huyo alijaribu kutoroka lakini
askari wakampiga risasi mkononi na mguuni akiwa juu ya ukuta, majeraha
hayo yalimfanya ashindwe kukimbia, akakamatwa.
Mahabusu huyo alifikishwa Mahakamani
kwa kosa la kufanya vurugu baada ya kulewa na hukumu yake ilikuwa alipe
faini ya Kshs 200, jaribio lake la kutoroka limefanya awe na kesi
nyingine mpya kutokana na kufanya kosa hilo.
Social Plugin