Jeshi
la polisi mkoani morogoro linamshikilia mtu mmoja Joseph Asenga
mwenye umri wa miaka 47 kwa tuhuma za kujifanya kuwa ni Padre wa kanisa
katoliki na hata kuendesha ibada.
Taarifa zilizothibitishwa na kamanda wa polisi mkoa wa
morogoro,Leonard Paulo, zimebainisha mtuhumiwa huyo kutiwa mbaroni
katika maeneo ya modeko katika kanisa katoliki la Mt.Maria ambapo
anadaiwa kuwahi kufika kanisani hapo kati ya Mei na Juni mwaka
jana,kabla ya kurudia tena hivi karibuni, akijitambulisha alikuwa padri
kwa kutoa vitambulisho feki akisema ametokea jimbo la NEW YORK nchini
marekani na alikuja nchini kwa mapumziko na katika upekuzi amekutwa na
majoho saba ya kipadri.
Katibu wa kanisa katoliki, jimbo katoliki la morogoro,Padre Lutsfud
Makseyo,amesema amelaani tukio hilo na kwamba limewasikitisha na
kuwahuzunisha kama kanisa,na kutoa wito kwa wananchi kushirikiana na
vyombo vya dola kuwafichua watu wote wanaofanya vitendo vya kitapeli kwa
kujihusisha na uongozi wa kiimani.
Social Plugin